Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameitangaza Kesho siku ya Alhamisi
Novemba 5 mwaka huu kuwa sikukuu na siku ya Mapumziko.
Rais Kikwete amefanya uamuzi huo ili
kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za Kuhitimisha Uongozi wa
Serikali ya Awamu ya nne na kukaribishwa madarakani Mheshimiwa Dokta John Pombe
Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa
Dar es Salaam leo na Ofisi ya Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Rais
Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa Mamlaka aliyonayo chini ya
Kifungu cha 3 cha sheria ya sikukuu za kitaifa.
No comments
Post a Comment