Na Peter Mkwavila,denis kazenzele
WANANCHI wa vijiji vya Chikola
Maghomanje na Nhgulugano wilayani Bahi mkoa wa Dodoma wanatarajia kufanya ibada
ya pamoja kumwomba Mungu ili watu waweze kuguswa kusaidia ujenzi wa daraja
lililokatika kwa mwaka mmoja.
Aidha pamoja na maombi hayo pia
wananchi hao watamshukuru mungu kwa kuwezesha uchaguzi kufanyika kwa amani
ikiwemo na ipatikanaji wa viongozi kwa njia ya amani pia.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi
hao wa vijiji hivyo Mchungaji wa kanisa la Angalikan Chikola Peter Fumbi
alisema maombi hayo yatafanyika kwa ajili ya kumomba mungu ili zipatikane fedha
zitazowezesha ujenzi wa daraja hilo.
Fumbi alisema kuwa jumla ya kiasi
cha zaidi ya shilingi milioni 300 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo,hivyo
kwa kupitia maombi hayo wanaamini fedha hizo zitapatikana.
Alisema kwa hivi sasa baada ya
kukatika kwa daraja hilo kumekuwepo na shida kubwa ikiwemo na kukosa huduma ya
kuwasafirisha wagonjwa wakiwemo wajawazito wanaotakiwa kupelekwa Hospitali ya
mkoa.
Aidha kero nyingine ya kukosekana
kwa daraja hilo ni pamoja na wanafunzi wanaotoka kijiji cha Chimendeli
kuja shule ya chikola sekondari kushindwa kuvuka pindi wanapokuta
maji yamejaa.
Hata hivyo mchungaji huyo alisema
kuwa mvua za masika zinakuja kuna hatari ya wananchi wakakosa huduma za
kimsingi kwa kuwa hawatakuwa na mawasiliano yoyote ya barabara kutokana na
kukatika kwa daraja hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji
cha Chikola Petro Masaka akizungumza na waandishi wa habarialisema kuwa maombi
hayo yatawashirikisha watu wote bila kujali itikadi zozote za kidini na vyama
vya siasa.
Masaka alisema kuwa ili kukamilika
daraja hilo tunahitaji nguvu za ziada kutoka kwa wahisani,watu binfsi hata na
kwa serikali pia.
No comments
Post a Comment