Hizi ni picha zikionesha mfano wa unyanyasaji wa kijinsia |
Dodoma
Wananchi mkoani Dodoma
wametakiwa kutumia siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya
kati yakihusisha mikoa ya Dodoma,Singida,Morogoro na Tabora.
Hayo yamezungumzwa na
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi:Chiku Gallawa kama mgeni rasmi katika ufunguzi wa
maadhimisho hayo yaliyofanyika leo katika viwanja vya Nyerere Square mjini
hapa.
Aidha kwa upande wake
kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime amezungumzia baadhi ya matendo ya
ukatili wa kijinsia na athari zake kwa jamii baada ya kutendeka.
Akizungumza na kituo
hiki kuhusu maadhimisho haya Bi:Mariam Kianga ambaye ni mkazi wa Manispaa ya
Dodoma amesema kuwa ushirikiano wa kila nyanja unahitajika ili kukomesha
maswala hayo yakiunyanyasaji yanayoendelea katika jamii.
Naye kwa upande wake Bw:Wilson
Mwangu amesema kila mwananchi ana wajibu kupinga na kuyazuia kuanzia ngazi ya
familia ili kumaliza vitendo hivyo.
Hata maadhimisho hayo
yanayofanywa kila mwaka ndani ya siku kumi na sita kupinga ukatili wa kijinsia kwa
kanda ya kati yameandaliwa na Shirika la AFNET kwa kushirikiana na Mtandao wa
kupambana na ukatili wa kijinsia(MKUKI) pamoja na Jeshi la Polisi yenye kauli
mbiu inayosema “FUNGUKA,CHUKUA HATUA,MLINDE MTOTO APATE ELIMU”.
No comments
Post a Comment