unaweza kupata habari zote hapa za kimataifa kupitia kazenzele1.blogspot.com au kupitia page ya denis kazenzele au omwatani hizi ni fb. |
South
Africa
Rais
wa Uchina Xi Jinping amesema taifa lake litatoa ufadhili wa dola bilioni 60 kwa
nchi za Afrika.
Tangazo
hilo amelitoa kwenye mkutano mkuu wa ushirikiano kati ya Uchina na nchi za bara
Afrika, ambao umeanza leo jijini Johannesburg. Viongozi kadha wa mataifa ya
Afrika wanahudhuria.
Tangazo
la fedha hizo za mabilioni ya dola ambazo zitatolewa kupitia ruzuku, mikopo na
ufadhili wa miradi ya maendeleo lilisubiriwa, lakini kiasi cha fedha
kilichoahidiwa kimezidi matarajio.
Sehemu
kubwa ya usaidizi huu wa kifedha sana utatolewa kupitia miradi ya miundo mbinu,
kusaidia kusisimua ukuaji wa kiuchumi, lakini maelezo zaidi hayajatolewa.
Kiongozi
mwenza wa mkutano huo Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesifu ushirikiano kati
ya Uchina na nchi za Afrika.
Amesema
watu wanaoishi Uchina na Afrika ni theluthi moja ya watu wote duniani, na
kwamba hilo ni soko kubwa la bidhaa.
Uchina,
nchi yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani, imetoa msururu wa mikopo kwa nchi
za Afrika, ambazo nazo huuzia taifa hilo mafuta na bidhaa nyingine muhimu.
Hata
hivyo, idadi ya bidhaa ambazo mataifa hayo huuzia Uchina imekuwa ikipungua.
Uwekezaji
wa Uchina Afrika ulishuka asilimia 40 nusu ya kwanza ya mwaka huu, kwa mujibu
wa wizara ya uchumi ya Uchina.
Ziara
ya Bw Xi barani Afrika imetazamwa na wengi kama hatua ya kuyahakikishia mataifa
ya Afrika kwamba Uchina itaendelea kuwekeza katika bara hilo licha ya kupungua
kasi kwa ukuaji wa uchumi wa Uchina.
Mapema
wiki hii Uchina na Afrika Kusini zilitia saini mikataba na mikopo ya thamani ya $6.5bn (£4.3bn), inayoangazia zaidi
miundo mbinu.
Jumla
ya mikataba 26 ilitiwa saini Jumatano, $2.5bn zikienda kwa shirika la reli la
serikali.
Kabla ya kutua Afrika Kusini, Bw Xi alizuru Zimbabwe Jumanne, ambako pia aliahidi taifa hilo
mikopo ya kusaidia kuinua uchumi wake uliodorora.
Bbcswahili
Gazeti la The Cairo Post linasema watu watatu waliokuwa wamejifunika nyuso zao walirusha bomu mgahawani na kisha kutoroka.
Shirika la habari la Reuters limemnukuu afisa mmoja wa usalama, ambaye hakutajwa jina lake, akisema mmoja wa washukiwa ni mfanyakazi wa zamani wa mgahawa huo.
Mgawaha huo ulikuwa ghorofa ya chini ya ardhi kwenye jengo hilo, jambo lililoifanya vigumu kwa watu kutoroka.
Wahasiriwa walifariki kutokana na majeraha ya moto au kwa kutokana na moshi. Watu watano wamejeruhiwa.
Mji wa Cairo umeshambuliwa mara kadha na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu.
Juhudi za wanamgambo hao wa Kiislamu zilizidi baada ya kung’olewa mamlakani kwa Rais Mohammed Morsi mwaka 2013.
Bbcswahili
Sita kati yao wanaripotiwa kuelekea maeneo ya kifahari ya Pattaya na Phuket huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.
Polisi nchini Thailand wanasema kwa hawajafanikiwa kuthibitisha uwepo wa raia hao wa Syria. Zaidi ya watu milioni moja unusu raia wa Urusi walizuru Thailand mwaka 2013.
Bbcswahili
Amesema wanawake sasa wanaweza kuendesha magari ya deraya, mizinga na kuongoza askari wa nchi kavu kwenye mapambano.
Mpango huo wa kiistoria unakwenda kinyume na hoja ya mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa majeshi kwamba Kikosi cha askari wa majini wanaweza kuruhusiwa kuwatenga wanawake katika baadhi ya majukumu kwenye mapambano ya mstari mbele vitani.
Bbcswahili
berlin
Jeshi la Ujerumani linatarajiwa kupeleka ndege sita
za upelelezi nchini Syria, kama sehemu ya muungano wa kimataifa katika
mapambano dhidi ya kundi lenye itikadi kali la Dola la Kiislamu-IS.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Ursula von der Leyen,
amethibitisha kuwa ndege za kujaza mafuta pia zitapelekwa nchini humo, pamoja
na manowari moja ya kuilinda manowari inayobeba ndege za kijeshi za Ufaransa.
Amesema mashambulizi ya anga na majeshi ya ardhini,
ulikuwa mkakati imara katika mapambano dhidi ya IS.
Aidha, wanajeshi 1,200 wa Ujerumani pia watapelekwa
Syria.
Von der Leyen amesema lengo la kuwepo kwa wanajeshi
hao watakaopelekwa mwezi Januari, ni kupambana na kukabiliana na IS, na kuwazuia
wanamgambo kufanya mashambulizi mengine ya kigaidi.
Bunge la Ujerumani leo
linatarajiwa kuidhinisha kupelekwa wanajeshi hao nchini Syria kupambana na IS.
dwswahili
Washington
Shirika la Upelelezi la
Marekani-FBI, linachunguza iwapo shambulizi la California lina uhusiano wowote
na vitendo vya kigaidi.
Siku ya Jumatano, watu 14 waliuawa
kwa kupigwa risasi na watu wawili waliokuwa na silaha nzito katika sherehe za
Krismasi zilizofanyika kwenye kituo cha kuwahudumia watu wenye ulemavu
kilichoko San Bernardino.
Maafisa wa kijasusi wameripoti kuwa
watu hao walikuwa wakifanya mawasiliano na wanamgambo wenye itikadi kali za
Kiislamu kupitia kwenye mtandao wa mawasiliano ya kijamii.
Polisi wamesema washambuliaji hao
walikuwa na risasi za kutosha na mabomu ya kuwaua mamia ya watu wakati
walipofanya shambulizi hilo.
Tangu kutokea kwa shambulizi hilo,
polisi wamepata mabomu na silaha nyingine katika nyumba ya washambuliaji.
Kutokana na shambulizi hilo, Rais
Barack Obama wa Marekani kwa mara nyingine tena amewatolea wito Wamarekani
kupitia upya sheria za kudhibiti matumizi ya bunduki.
Dwswahili
Nairobi
Serikali itapoteza jumla ya shilingi bilioni 60 zinazotokana
na maua mboga na matunda yanayozwa katika mataifa ya kingeni, baada ya mataifa
ya Uropa kuanza kutekeleza sheria mpya kuhusu bidhaa zinazouzwa nchini humo.
Meneja wa muungano wa wauzaji wa mboga maua na matunda Francis Wario ameishauri serikali kuwaelimisha wakulima wa bidhaa hizo kuhusu kemikali zilizoidhinishwa ili kuzuia bidhaa zinazotoka humu nchini kupigwa marufuku Uropa.
Cri
No comments
Post a Comment