URUSI
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Uturuki itajuta zaidi ya mara moja kuhusiana na hatua yake ya kuiangusha ndege ya kijeshi ya Urusi karibu na mpaka kati ya Syria na Uturuki, akiongeza kwamba hata puuzia hatua ya Uturuki ya kuwasaidia magaidi.
Ameishutumu Uturuki kwa kununua mafuta kutoka kwa kundi la Dola la Kiislamu, na kuongeza kwamba hatua ya Uturuki kuiangusha ndege ya Urusi ni sawa na uhalifu wa kivita.
Katika maelezo yenye kulenga mataifa ya magharibi, Putin amesema katika hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa hilo kwamba nchi hazipaswi kufanya unafiki kuhusiana na ugaidi, ama kuyatumia makundi ya kigaidi kwa maslahi yao.
Rais Putin ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuja pamoja kupambana na ugaidi.
dwswahili
MAREKANI
Polisi nchini Marekani jana imewatambua washukiwa wawili, mwanamume na mwanamke , ambao wameuwawa katika majibishano ya risasi na polisi kufuatia mashambulizi ya bunduki ambapo watu 14 waliuwawa na wengine 17 walijeruhiwa jimboni Califonia.
Mkuu wa polisi wa mji wa San Benardino Jarrod Burguan amesema polisi haiamini tena kwamba mshukiwa wa tatu amekimbia na kusema wana imani kwamba watu wawili waliofyatua risasi katika jengo ndio hao waliouwawa.
Wa kwanza ni Syed Rizwan Farook , mwenye umri wa miaka 28, mzaliwa wa Marekani na wa pili ni Tashfeen Malik mwanamke mwenye umri wa miaka 27.
Burguan amesema Farook alikuwa ni mfanyakazi wa serikali kwa muda wa miaka mitano kama mtaalamu wa masuala ya mazingira katika idara ya afya.
Rais barack Obama ametoa wito wa kuchukuliwa juhudi za kupambana na matukio ya mauaji kama hayo nchini humo.
Bbcswahili
**************************************************************
Kansela Angela Merkel na rais wa Afghanistan Ashraf Ghani wamekuwa na mazungumzo mjini Berlin jana.
Majadiliano yao yalituwama zaidi katika masuala ya wakimbizi , ambapo kansela Merkel amesema kwamba Waafghanistan wanaokuja nchini Ujerumani wakitafuta hali bora ya kiuchumi watarejeshwa nyumbani.
Ameongeza kwamba watu ambao bado wako nchini humo wanapaswa kusogea katika maeneo salama badala ya kuhamia barani Ulaya.
Zaidi ya Waafghanistan 140,000 wameikimbia nchi yao mwaka huu wakihofia usalama wao na mashambulizi ya wanamgambo wa Taliban. Wengi wa wale walioikimbia nchi hiyo wameingia nchini Ujerumani.
Akizungumza katika mkutano na waandishi habari pamoja na rais Ghani wa Afghanistan , Merkel amesema Ujerumani itatimiza wajibu wake wa kiutu kwa Waafghanistan ambao wako katika hatari kubwa kwasababu wanafanyakazi na majeshi ya kigeni kama jeshi la Ujerumani.
Dwswahili
******************************************************************
ENGLAND
Ndege za kijeshi za Uingereza
zimetekeleza mashambulio ya angani dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria
saa chache baada ya bunge kuidhinisha mashambulio hayo, Wizara ya Ulinzi ya
Uingereza imethibitisha.
Duru za serikali zimesema ndege hizo
tayari zimerejea kambini katika visiwa vya Cyprus.
Awali, wabunge nchini Uingereza
walikuwa wamepiga kura kwa wingi kuunga mkono mashambulio hayo, wabunge 397
wakiunga mkono dhidi ya 223, baada ya mjadala mkali uliodumu saa 10 katika
bunge la Commons.
Jumla ya wabunge 66 wa chama cha
Labour waliunga mkono serikali huku David Cameron akipiata kura nyingi kuliko
ilivyotarajiwa katika bunge hilo.
Waziri Mkuu huyo alisema amechukua
“hatua ifaayo kuweka taifa salama” lakini wapinzani wake walisema hilo ni kosa.
Ndege nne za kijeshi ziliripotiwa
kupaa kutoka kambi ya kijeshi ya RAF Akrotiri, Cyprus, baada ya kura hiyo
kupigwa.
Ndege nyingine nne zilikuwa tayari
kupaa kutoka kambi hiyo, ambayo imekuwa ikitumiwa kutekeleza mashambulio nchini
Iraq.
Mbili kati ya ndege hizo nne aina ya
Tornado zilirejea Cyprus saa tatu baadaye.
Taarifa zinasema jeshi la wanahewa
la Uingereza, maarufu kama RAF, “limekuwa likijiandaa kuhusika katika
mashambulio hayo, kujiunga na mataifa mengine ya muungano yanayokabiliana na IS
nchini Syria, “kwa miezi kadha”.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha
Labour Jeremy Corbyn alipinga mashambulio hayo lakini chama chake
kiligawanyika, baadhi ya viongozi wake wakuu wakijitenga na msimamo wake.
Bbcswahili
********************************************************************
SUDANI
Herve
Ladsous, mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa amesema kuwa
mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi Agosti kati ya pande hasimu za Sudan
Kusini yamefikia hatua nyeti.
Mapatano
hayo yameshindwa kutatua tofauti kubwa zilizopo kati ya wafuasi wa Rais Salva
Kiir wa nchi hiyo na waungaji mkono wa aliyekuwa makamu wake, Riek Machar.
Herve
Ladsous ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mapatano
yaliyofikiwa kati ya pande mbili hizo hasimu yanatekelezwa kwa mwendo wa
kinyonga jambo ambalo linahatarisha amani na usalama katika nchi hiyo change
zaidi barani Afrika.
Maelfu
ya watu wameuawa na wengine milioni 2.3 kulazimika kuishi kama wakimbizi ndani
na nje ya nchi hiyo tokea ijitenge na Sudan.
Wakati
huohuo Bani Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba mivutano na
chuki za jadi zilizopo kati ya pande hasimu huko Sudan Kusini zinaweza kuzua
wimbi kubwa la mauaji na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Watu
wapatao milioni 4.6 wa nchi hiyo wanakabiliwa na baa la njaa na wanahitajia
misaada ya dharura ya chakula ili kuwaepusha na maafa yanayowakabili.
Iribswahili
****************************************************************************
Faini hiyo ilimlazimisha mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo kujiuzulu na mauzo ya hisa ya kampuni kudorora.
Lakini kufuatia wiki kadhaa za majadiliano utawala umekubali kupunguza faini hiyo.
Faini hiyo ambayo inahitaji kulipwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ni zaidi ya faida ya mwaka mmoja ya MTN nchini Nigeria.
Nigeria imekuwa ikilazimisha makampuni ya mawasiliano kuwasajili wateja wao kutokana na hofu kuwa, kadi ambazo hazijasajiliwa zinaweza kutumiwa na makundi ya kigaidi na wahalifu.
BBCSWAHILI
No comments
Post a Comment