Habari
Kutokana na mzozo baina ya
wafanyabiashara wa soko kuu la majengo mkoani hapa na manispaa uliodumu sasa
kwa siku kadhaa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma,Clemens
Mkusa ametoa siku tano kwa ajili ya ukarabati wa mtaro wa maji machafu uliopo
katikati ya Soko hilo kwani wasipofanya hivyo vibanda vilivyopo kandokando
vitavunjwa.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya
juzi jumanne Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri MkuuTawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI)Jumanne Sagini kufanya ziara ya dharura katika soko hilo na
kuamuru baadhi ya vibanda vibomolewe ili kutoa nafasi ya kufanya usafi
katika mfereji wa soko hilo.
Akizungumza Mjini hapa na
viongozi wa Wafanyabiashara katika kikao kilichofanyika katika ofisi za
Manispaa,Kaimu Mkurugenzi huyo amesema wamewapa siku tano za kuhakikisha mtaro
huo unakuwa safi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja
wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo,Godson Rugazama amesema wapo tayari
kutii agizo la serikali katika kuweka mazingira ya usafi kwenye mtaro huo.
Amesema kilichokuwepo ni kutupiana
mzigo kati ya Mamlaka ya ustawishaji Makao Makuu (CDA) na Manispaa ni nani
mwenye mamlaka ya kufanya usafi wa mtaro.
Amesema mara baada ya kuonekana CDA
ndio wenye mamlaka,Manispaa hawakuwapatia fedha za kusafisha mtaro huo hali
iliyofanya mrundikano wa uchafu katika eneo hilo.
Hata hivyo
katika makubaliano yao imeonekana kuwa wafanyabiashara hao wametii amri hiyo
mara baada ya jana siku ya alhamis kuonekana wakisafisha mfereji huo huku
wakidai kuwa katika makubaliano yao ni kwamba unapashwa kuwa safi kabla ya
disemba 9 ambayo ndio siku ya uhuru, siku ambayo imevunjwa kwa maana hiyo
kutakuwepo na zoezi la usafi kwa nchi nzima ikiwemo mkoani hapa ambapo kwa siku
kadhaa hivi sasa usafi wa mazingira umekuwa ukiendelea huku watumishi
wanaokwenda kinyume na matakwa ya viongozi wa juu yao wamekuwa wakiambulia
vibao.
ukiachana na hilo pia hapa chini nimekuwekea sauti ya Anthony Mavunde akizungumzia suala hilo na kutoa suluhisho>>>>biinyeza hapa chini
No comments
Post a Comment