Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
KARONGA: Watanzania wanane wametiwa nguvuni na serikali ya Malawi wakituhumiwa kufanya upepelezi katika mgodi wa madini ya Uranium uliopo Kayelekera, wilayani Karonga, mji ulio mpakani na Kyela nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya Malawi, watu hao wanadaiwa kufanya upelelezi wa mgodi huo, wakiamini eneo hilo lilikuwa likitengeneza silaha za nyuklia na kwamba walikuwa ni wananchi wa Kalonga ndiyo waliowatilia mashaka na kuwaita polisi waliowakamata.
Msemaji wa jeshi la Polisi wa Karonga, George Mlewa alikaririwa akithibitisha kukamatwa kwa watu hao na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea dhidi yao huku wakichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa mahabusu huko Mzuzu.
Hivi karibuni kundi la wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka Tanzania waliokwenda kwa mwaliko wa kanisa la Moravian, walizuiwa kutembelea mgodi huo.
Chanzo: Global Publisher
No comments
Post a Comment