Michuano hiyo Inaanza hapo kesho huko nchini Japan.
Vijana hao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walishinda kombe la klabu bingwa Afrika mwezi uliopita.
Wataanza kampeni yao Osaka Jumapili dhidi ya mshindi wa mechi kati ya Sanfrecce Hiroshima na Auckland City FC ambayo itachezwa Alhamisi.
Mazembe walishangaza ulimwengu miaka mitano iliyopita walipofika fainali ya dimba hilo la dunia lakini wakashindwa na Inter Milan.
UEFA
Baada y ahapo jana kushuhudia moja
ya timu zoefu kwenye mashindano ya UEFA ikiaga mashindano hayo{ Man united} leo
hii pia tunatarajia kuona timu nyingine nyingi zikifanikiwa kusonga na nyingine
nyingi zikiondolewa au kutupwa UEFA ndogo, Je! Chelsea, Arsenal, Psg Zitasonga
au ndo kama man U kukimbilia EUROPA LEAGUE?
Hizi hapa ndizo zinazojimwaga leo
usiku
Bayer Leverkusen ? - ? Barcelona
Roma ? - ? BATE Borisov
Dinamo Zagreb ? - ? Bayern Munich
Olympiacos ? - ? Arsenal
Chelsea ? - ? FC Porto
Dynamo Kyiv ? - ? Maccabi Tel Aviv
Gent ? - ? Zenit St. Petersburg
Valencia ? - ? Lyon
*******************************************************************
SCHWEINSTEIGER
Schweinsteiger amepewa hadi Alhamisi Saa 9 Mchana kukana au kukubali Mashitaka.
Refa wa Mechi hiyo, Mark Clattenburg, hakulitaja tukio hilo lakini aliongea na Wachezaji wote Wawili baada ya tukio lenyewe.
Katika Taarifa yao, FA imesema kuwa tukio hilo lilipitiwa na Marefa Watatu tofauti ambao kila mmoja aliafiki lilistahili Kadi Nyekundu na ndio maana wakafungua Mashitaka dhidi ya Schweinsteiger.
Laiti kama Refa Mark Clattenburg angelilitaja tukio hilo kwenye ripoti yake ya Mechi basi FA isingekuwa tena na mamlaka ya kulipitia na kumshitaki.
Ikiwa Schweinsteiger atafungiwa Mechi 3 atazikosa Mechi za Ligi dhidi ya Bournemouth, Norwich City na Stoke City na kurejea kwenye Mechi na Chelsea.
**********************************************
NBA MAREKANI - JANA
Charlotte Hornets 104 Detroit Pistons 84
Philadelphia 76ers 68 San Antonio Spurs 119
Miami Heat 103 Washington
Wizards 114
New York Knicks 97 Dallas
Mavericks 104
Toronto Raptors 102 L. A. Lakers 93
Chicago Bulls 101 Phoenix
Suns 103
Milwaukee Bucks 90 Portland Trail Blazers 88
Minnesota Timberwolves 106 L.
A. Clippers 110
New Orleans Pelicans 93 Boston Celtics 111
NBA
LEO
Cleveland Cavaliers 105 Portland Trail Blazers 100
Indiana Pacers 123 Golden
State Warriors 131
Brooklyn Nets 110 Houston Rockets 105
Memphis Grizzlies 88 Oklahoma
City Thunder 125
Denver Nuggets 74 Orlando
Magic 85
Sacramento Kings 114 Utah Jazz
106
NBA KESHO - December
10
03:00 Boston Celtics VS Chicago Bulls
03:00 Charlotte Hornets VS Miami
Heat
03:00 Washington Wizards VS Houston
Rockets
03:30 Detroit Pistons VS Memphis
Grizzlies
03:30 Toronto Raptors VS San Antonio
Spurs
04:00 Milwaukee Bucks VS L. A.
Clippers
04:00 Minnesota Timberwolves VS L.
A. Lakers
05:00 Phoenix Suns VS Orlando Magic
05:00 Utah Jazz VS New York Knicks
05:30 Dallas Mavericks VS Atlanta Hawks
***********************************************************
Kisa na maana shirikisho la kimataifa la masumbwi IBF lilikuwa linataka apiganaje na mpinzani wake anayepigiwa upatu Vyacheslav Glazkov kabla ya kupigana na bondia yeyote yule.
Hata hivyo Fury aliyewatamausha wapenzi wa ndondi za uzani mzito kwa kumchapa bondia kutoka Ukraine Wladimir Klitschko na kutwaa mataji yote matatu ya ndondi ya IBF WBA na WBO.
Pigano hilo la Novemba tarehe 28 lilitamatisha udhibiti wa raia huyo wa Ukraine wa mikanda yote 3 ya ndondi iliokuwa imedumu kwa zaidi ya miaka 10.
Yamkini Fury alilazimika kupigana dhidi ya Wladimir Klitschko kutokana na kipenge cha mkataba waliotia sahihi na bondia huyo wa Ukraine.
Mwenyekiti wa shirikisho la ndondi la kimatafa IBF Lindsey Tucker, amethibitisha kuwa Fury amepokonywa ukanda huo wa uzani mzito.
Fury ambaye ameshinda mapigano 25 ya kulipwa amesalia na mikanda miwili ya WBA na ile ya WBO.
Ukanda mwngine wa uzani wa juu WBC unashikiliwa na bondia kutoka Marekani Deontay Wilder.
Kimsingi Ukanda huo wa IBF unarejea Ukraine kwani Glazkov, mwenye umri wa miaka 31 ni raia wa Ukraine,na ameshinda mapigano 21 kati ya 22 alizoshiriki.
*****************************************************************
MOURINHO
VS ABRAMOVICH
Akiongea kuelekea Mechi hii ya UCL, Mourinho, alipoulizwa kama atabakishwa kama Meneja wa Chelsea, alijibu: “Nadhani nimefanya mengi mazuri kwa Klabu hii. Sidhani Mmiliki ni Mtu anaeyumbayumba.”
Mourinho, ambae ni Mreno leo Jumatano anapambana na Klabu ya kwao Ureno FC Porto ambayo aliwahi kuwa Kocha wao, ameeleza: “Abaramovich ameniamini mara mbili.
Huku kukiwa na uvumi kuwa Mourinho atatimuliwa ikiwa atafungwa Mechi mbili mfululizo na Mechi ya leo na FC Porto na kufuatia fuatia kipigo cha Bournemouth, kwenye Mechi ya Ligi Jumamosi iliyopita.
Jumatatu ijayo, Chelsea itacheza na Vinara wa Ligi Leicester City.
Hii ni himaya ya Pili ya Mourinho akiwa na Chelsea baada ya kujiunga nayo tena Mwaka 2013 na kutwaa Ubingwa wa England na Capital One Cup.
Mara ya kwanza kuwa na Chelsea ilikuwa kati ya 2004 na 2007 ambapo alitwaa Ubingwa wa Ligi mara 2 FA CUP na Kombe la Ligi mara 2.
No comments
Post a Comment