Kadhalika, jarida hilo limetaja kuingia kwa Urusi nchini Ukraine.
Bi Merkel ametoa “uongozi wa busara katika ulimwengu ambao umepungukiwa”, mhariri wa jarida hilo Nancy Gibbs ameandika.
Kiongozi wa kundi la wapiganaji linalojiita Islamic State Abu Bakr al-Baghdadi ametajwa kuwa wa pili, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Donald Trump, anayesaka tiketi ya kuwania urais Marekani kupitia chama cha Republican.
Bi Merkel amejiunga na washindi wa awali wakiwemo Adolf Hitler, Joseph Stalin, Mahatma Gandhi, Winston Churchill na Richard Nixon.
Tuzo ya mwaka jana ilikabidhiwa matabibu waliosaidia kukabilina na mkurupuko wa Ebola Afrika Magharibi. |
No comments
Post a Comment