DODOMA
Serikali wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma imekanusha
taarifa za watu wa
wilayani hapo kuchemsha mawe kwa ajili ya kukosa chakula kutokana na kukikdhili
kwa njaa.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati ya maafa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mwl,Mohamed Utaly alipokuwa ikitoa taarifa ya hali ya njaa kwa mkurugenzi wa idara ya uratibu wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya.
Mwl.Utaly amesema kuna vyombo vya habari na
mitandao ya kijamii imeripoti kuwa wananchi wa wilaya ya mpwapwa
hulazimika kupika mawe na pumba kwa ajili ya kujikimu na njaa
kutokana na wilaya hiyo kukubwa na njaa kwa hali ya juu.
Aidha Mwl.Utaly amekili kuwepo kwa hali ya
njaa katika wilaya hiyo lakini alisema haiko kwa kiasi ambacho
kimelipotiwa katika vyombo vya habari hadi wananchi kupika mawe na pumba
.
Mmoja wa wa wananchi wa kijiji cha
Chunyu bwana Edward Kusena ambae
ni mkulima mkuubwa wa zao la mhogo kijiji hapo amesema njaa katika kijiji hicho na wilaya nzima imesababishwa na baadhi wananchi kuupuzia maagizo ya wataalamu ya kulima mazao yanayo stahimili ukame na yanayo komaa haraka kama mhogo,matama na uwele kwa wilaya zenye mvua kidogo kama Mpwapwa.
ni mkulima mkuubwa wa zao la mhogo kijiji hapo amesema njaa katika kijiji hicho na wilaya nzima imesababishwa na baadhi wananchi kuupuzia maagizo ya wataalamu ya kulima mazao yanayo stahimili ukame na yanayo komaa haraka kama mhogo,matama na uwele kwa wilaya zenye mvua kidogo kama Mpwapwa.
Afisa kilimo, uvuvi na umwagiliaji wa wilaya
ya Mpwapwa Bi Justina Munisi alisema pamoja na kuwapo kwanjaa tayari
kitengo cha maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu imetoa mahindi tani 200 ambayo
tayari yamesha gawiwa kwa vijiji 36 kati ya vijiji68 vilivyo athiliwa na njaa kwa
kiasi kikubwa.
Bi Munis alisema njaa hiyo imesababishwa
na na ukosefu wa mvua kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2014/2015,na
wananchi kuto kufuata mazao yanayo stahili kupadwa katika kanda za mikoa ya
ukame kama Dodoma na wilaya zake.
Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya maafa ofisi ya waziri mkuu brigedia Jenaerali Mbazi Msuya aliwataka viogozi w halmashauri hiyo kuacha kuomba chakula cha msaada bali aiwataka kuomba chakula cha njaa na mbegu ili kuweza kondokana na kuomba chakula cha njaa kila mwaka.
Pia alisema kitengo chake kitaanza kugawa mbegu za mhogo bure kwa wakulima watakao jiandikisha na kutaka kupanda zao hilo ambalo litaweza kuwa mwaraobaini wa wilaya hiyo kukubwa na njaa kila mwaka.
Chanzo Luitiko Noel - mpwapwa.
No comments
Post a Comment