Rais Paul Kagame wa Rwanda ametangaza leo nia yake ya kugombea muhula wa
tatu katika uchaguzi wa mwaka wa 2017, huku akithibitisha uamuzi
uliotarajiwa na wengi kufuatia kuidhinishwa kwa marekebisho ya katiba
ambayo yanaweza kumruhusu kusalia madarakani kwa miaka mingi ijayo.
Akizungumza katika hotuba iliyorushwa na televisheni, Kagame amewaambia wananchi kuwa ameitikia wito wao wa kumtaka awanie muhula mwingine hapo mwaka wa 2017.
Hata hivyo, amesema Rwanda haihitaji kiongozi wa milele.
Kagame amekuwa madarakani tangu mwaka wa 2000, akiwa anadhibiti takribani kila muhimili wa utawala tangu jeshi lake la waasi lilipoingia mjini Kigali kusitisha mauaji ya halaiki ya mwaka wa 1994.

No comments
Post a Comment