Vijana
wametakiwa kuwa mabalozi wa mabadiliko ili kuweza kuondoa dhana iliyojengeka
katika jamii kuwa mambo yote mabaya yanayotokea katika jamii wao ndio wahusika wakuu
wa mambo hayo.
Kauli hiyo
imetolewa na mtaalamu wa maswala ya vijana na ujasiriamali Joseph Kaphinga wakati akiwasilisha mada inayohusu
vijana na ujana iliyofanyika mjini
Dodoma chini ya mpango wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya AIRTEL
ujulikanao kama AIRTEL FULSA TUNAWAWEZESHA.
Kaphinga amesema kundi la vijana limekuwa
haliaminiki katika jamii kutokana na vijana walio wengi kujihusisha na utumiaji
na usafirishaji wa madawa ya kulevywa, wizi
kutoa mimba ngono zembe na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Kwa upande
wake Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi amesema asilimia kubwa ya watanzania ni vijana hivyo vijana wanatakiwa kuzichangamkia Fulsa
zinazojitokeza na kuzitumia vizuri ili waweze kujikwamua kiuchumi ikiwemo
kujiaminisha kwa makundi mengine kuwa wanaweza kuchangia pato la taifa kwa
kiasi kikubwa.
Airtel
Tanzania imeanzisha mpango wa kuwawezesha vijana kuanzia umri wa miaka 18 hadi 24 kutokana na kuamini kuwa kundi hilo ndilo
lenye uwezo na nguvu nyingi za kuleta mabadiliko ya kiuchumi kuliko kundi linguine
nchini
LYDIA
KISHIA/ BANDA
No comments
Post a Comment