NA: JOHN BANDA
..................................
Fedha zilizotolewa na mfuko wa Tasaf awamu ya tatu kwa ajilia ya kunusuru kaya maskini katika wilaya ya Ludewa
zimeanza kuonyesha mafanikio kwa walengwa na kubadilisha maisha yao kwa kuanza
kuuaga umaskini ikiwa ni miezi michache baada ya kuzana kutolewa.
Zlizotolewa kwa kaya maskini 3174
zimeanza kuonyesha mafanikio kwa walengwa kuondokana na umaskini kwa
kujishughulisha na ufugaji kuku, nguruwe na wengine kuanza ujenzi wa nyumba
bora za kuishi.
Anes Nyangonyara, Mona Haule, Michael Haule ni Wanufaika wanashuhudia
mabadiliko baada ya kupata fedha jinsi zilivyo badilisha maisha yao.
Mratibu wa Tasaf wilaya hiyo William Malima anaelezea idadi
wanufaika wa fedha za Tasaf katika kijiji cha Ludewa vijijini na jinsi walivyo
badilisha maisha yao huku makamu mwenyekiti akitoa wito wa kuongeza misaada.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Rehema Nchimbi amewagiza maafisa ugani katika mkoa wa Njombe
kuwatembelea wanufaika wa Tasaf ili kuwapa msaada kwa walipo fikia.
No comments
Post a Comment