John banda Njombe
MAMA
na wajomba wawili wa Mtoto Peter Mturua wakazi wa Igagala halmashauri
ya Wanging’ombe, wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mauaji ya mtoto
wao huyo kwa kuiba pesa na betri ya solar.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Njombe Wilbrod Mutafungwa amemtaja mama huyo kuwa ni
Devota Mhagama (38), na wajomba ni Motestu Mwajombe (26), na Wilium
Msigwa (18) wakazi wa kijiji cha Igagala kata ya Ulembwe wilaya ya
Wanging’ombe.
Akisimulia
kisa cha kuuawa Peter amesema kuwa mtoto huyo aliuwawa Disemba 23,
mwaka huu majira ya saa 1:40 usiku, mtoto huyo alituhumiwa kuiba
shilingi 40,000 na betri ya sola ambayo alikuwa akitumia mama yake
nyumbani kwao.
Alisema
kuwa marehemu alipigwa kwa kuchangiwa na Mama, wajomba na kusababisha
kifo chake baada ya kubaini kuwa pesa zilizo kuwa zimehifadhiwa na mama
yake na kusema kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani uchunguzi
ukikamilika.
Na John Banda
No comments
Post a Comment