DODOMA
ZIKIWA zimebaki siku chache kwa shule za msingi na
sekondari kufunguliwa mpaka sasa wazazi
na walezi wa wanafunzi mkoani Dodoma bado wapo katika hali ya sintofahamu
kutokana na kutojua kiwango halisi cha ada hasa katika shule Binafsi ambapo serikali
ilishatanga kufuta ada na michango mbalimbali katika shule zake.
Wakizungumza kwa nyakati Tofaiuti na Rasi Fm mjini
Dodoma wazazi hao wamesema zimebakia
siku chache bado hawajajua viwango vya
ada kwa shule binafsi hali inayowapa ugumu wa kufanya bajeti zao.
kwa upande
wake Felichesmi Peter ameiomba serekali kutaja ada ili kuwapa nafasi wazazi kuandaa ada hiyo kwa kiasi husika na wakati
sahihi.
Wananchi hao wametoa utofauti wa viwango vya elimu vinavyopatika
shule za serekali na zabinafsi
Hivi Karibuni Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya
Dkt, John Pombe Magufuli ilitangaza kufuta ada na michango mingine kwa shule
zake za msingi na Sekondari huku ikitoa ikitangaza Ada Elekezi kwa wamiliki wa
shule Binafsi.
John Banda
No comments
Post a Comment