Hali ya usalama katika mji wa London siku moja kabla ya mkesha wa mwaka
mpya imeimarishwa, huku hali ya tahadhari ya usalama ikiendelea kuwa ya
juu.
Kwa kawaida mji wa London hukaribisha mwaka mpya kwa tamasha la fataki linalovutia maelfu ya watu.
Kamanda wa polisi wa London Jo Edwards anasema,"kutakuwa na polisi elfu 3 mjini London wakati wa mkesha wa mwaka mpya, watu wataona ongezeko la idadi ya polisi ikiwezekana na polisi wenye silaha, ikiwa ni pamoja na wale wa London na wanaolinda usalama kwenye usafiri watakuwa na mipango yao ya kuimairsha usalama kwenye vituo vya usafiri nao pia watakuwa na silaha"
Kwingineko mjini Brussels nchini Ubelgiji usalama umeimarishwa baada ya polisi kuwakamata watuhumiwa wawili wanaodhaniwa kutaka kufanya shambulizi. Msemaji wa serikali ya Ubelgiji amesema hakuna silaha zilizokamatwa, lakini mavazi ya kijeshi nyaraka za uchochezi za kundi la IS zilikamatwa.

No comments
Post a Comment