CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzabar kimeipongeza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli aliyohutubia Taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa juma lililopita ikielezea mafanikio ya siku mia moja za uongozi wa Kiongozi huyo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Vuai Ali Vuai ametoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza na
Wanahabari hapo Afisini kwake, Kisiwandui mjini Unguja.
Amesema kwamba serikali ya awamu
ya tano imeonyesha nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wote bila ya
ubaguzi, hali inayopelekea mamia ya Watanzania kuendelea kuiamini CCM
kwamba ni chama cha wananchi wote kisichoongozwa kwa misingi ya
matabaka.
Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM
Zanzibar alisema hotuba hiyo ya Dr Magufuli ilijaa kila aina ya
uzalendo na nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania hasa wanyonge na
kuonyesha dhamira ya kweli ya utendaji wa taasisi za umma kwa manufaa
ya wananchi.
“ Tunampongeza Rais wa Jamguri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.Magufuli pamoja na wasaidizi wake, kwa hotuba
yake iliyojaa busara, hekima, ukomavu wa kisiasa na kuongeza kuwa ni
dira ya mafanikio yaliyotukuka katika nyanja mbali mbali za kiuchumi,
kijamii na kisisasa”. Alidai Vuai.
“Pia tunawaomba watendaji wa
serikali na taasisi binafsi kuendelea kuwaunga mkono viongozo hao, ili
Tanzania iweze kufikia nia yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati katika
miaka michache ijayo, na hilo linawezekana endapo kila mtu atafanya
kazi kwa uzalendo na weledi wa nafasi anayoitumikia.”. alikazia Naibu
katibu Mkuu huyo.
Vuai alisisitiza haja kwa
wananchi kuwa mstari wa mbele katika kubuni na kupanga mikakati
itakayosaidi kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi na kamwe halitakiwi
kuchanganywa na itikadi za kisiasa.
Akizungumzia suala la marudio ya
uchaguzi mkuu wa uliopangwa kufanyika Machi 20, Vuai alisema ni uamuzi
wa busara na wa kikatiba wa Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na
Zanzibar ya mwaka 1984 na kuongeza kusema hakika yeye hana mamlaka
kisheria ya kuingilia maamuzi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar, kwani ni
chombo huru kama vilivyo Tume nyengine za Uchaguzi duniani.
“Dkt. Magufuli ameweka wazi
kabisa kuhusu kile kinachodaiwa ati kuwa ni mgogoro wa uchaguzi wa
marudio kwamba hawezi kuingilia Maamuzi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar,
ambayo ipo kikatiba na ina Mamlaka kamili kama zilivyo Tume zingine za
uchaguzi duniani, hivyo haitakiwi kuingiliwa na maamuzi yake”.
Alifafanua Vuai.
Naibu Katibu Mkuu huyo,
alivitolea wito vyomba vya habari hapa nchi kutopotosha umma hasa wakati
huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa marudio ulitajwa kufanyika
Machi 20, mwaka huu.
VUAI alitoa wito huo kwa vyomba
vya habari kufuatia baadhi ya magazeti kuandika habari za upotoshaji
kuwa “vyama 10 vyaigomea Tume ya Uchaguzi Zanzibar kushiriki uchaguzi
mkuu wa marudio Visiwani Zanzibar”.
Alisisitiza haja kwa wanahabari
kutambua kuwa baadhi ya vyama vya UPDP na UMD vilivyotajwa kutoshiriki
kwenye uchaguzi wa marudio, havikuweka wagombea wake katika uchaguzi
uliopita hapo Oktoba 25, na kuvihusisha kutoshariki kwa uchaguzi wa
marudio kinalenga kukuza idadi ya vyama na hivyo kufanya usanii mkubwa
wa kisiasa.
Vuai amevitaja vyama
vilivyosimamisha wagombea ni 14 ambavyo ni CCM, CUF, SAU,TLP,ACT
Wazalendo, ADC, TADEA, AFP, CHAUMMA, Demokrasia makini, DP, Jahazi
Asilia, NRA na TLP.
Kupitia mkutano huo, Naibu
Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar, amewahimiza wananchi wote wapenda
amani na utulivu wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
Uchaguzi Mkuu wa Marudio Visiwani Zanzibar, kwani hiyo ni haki yao ya
msingi kikatiba na kidemokrasia.
No comments
Post a Comment