Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) Jumamosi kati ya watani wa jadi Simba SC dhidi ya Yanga SC
utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku kiingilio cha
chini kikiwa ni Shilingi elfu saba tu (7,000).
Kiingilio cha juu cha mchezo huo
kitakua shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini
(20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya
machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na
kijani.
Tiketi za mchezo huo zitaanza
kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya TFF
(Karume), Buguruni Olicom, Ubungo Oilcom, Kidongo Chekundu (Mnazi
Mmoja), Posta (Agip), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Taifa, Makumbusho
Stand, Kivukoni Ferry.
Mchezo huo utachezeshwa na
waamuzi wote wenye beji za FIFA, mwamuzi wa katikati Jonesia Rukyaa
(Kagera), akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha),
mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) huku Kamisaa wa mchezo huo akiwa
Khalid Bitebo (Mwanza).
Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea
Jumamosi kwa michezo sita, Young Africans v Simba (Taifa), Mbeya City v
Azam (Sokoine), Stand United v JKT Ruvu (Kambarage), Toto Africans v
Kagera Sugar (CCM Kirumba), Mgambo Shooting v Tanzania Prisons
(Mkwakwani) na Majimaji FC v Mtibwa Sugar (Majimaji).
Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa
michezo miwili, Mwadui FC v Coastal Union uwanja wa Mwadui Complex,
huku Ndanda FC wakicheza dhidi ya African Sports uwanja wa Nagwanda
Sijaon mjini Mtwara.
No comments
Post a Comment