Joyce Fundi miaka 982) mwenye Jembe akieleza jambo kuhusu Makaburi hayo na Jinsi shamba lake pamoja na ya wakulima wengine yalihatalini kutaifishwa. IMETENGENEZWA NA BANDA BLOG |
Moja ya Kaburi lililopo katika Mashamba hayo yenye Mgogoro katika ya wakazi wa Mapinduzi na Mwenzao kijini hapo, Kaburi hilo lilizikwa mwak 1958 |
Baadhi ya wakulima wa Kijiji cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika katika Eneo la Mgogoro ambalo walikuwa wakilitumia kwa kilimo. |
Na John Banda, Dodoma
ZAIDI ya Wakulima 60 wa Kijiji cha Mapinduzi ‘A’ kata ya Nghong’onha manispaa ya Dodoma wanawasiwasi wa
kunyang’anywa mashamba yao yenye ukubwa wa Hekari 237 kutokana na mkazi mwenzao
aliye na nia ya kuwadhulumu kwa vitisho vya kutumia polisi ikiwemo kuburuzwa
mahakamani huku wakikosa msaada wowote toka kwa viongozi wa ngazi za juu.
Wakizungumza na waandishi wa habari Kijijini hapo wakulima
hao walisema wamekuwa wakipata wakati mgumu tangu mwaka 2012 ambapo Bwana
Mchiwa Chedego alipowaomba wamuuzie mashamba ili ayatumie kwa kilimo cha zabibu
wakamkatalia na ndipo akaanza visa vya kuwakamata na kuwapeleka kwenye mabaraza
ya ardhi ngazi za kijiji na kata ambako walishinda na baadae akawahamishia
Wilayani.
Kwa upande wake George Chidawili (91) alisema walipopelekwa
baraza hilo la Ardhi la Wilaya walishangaa wameongezeka mpaka kufikia 11 na
baadae kuongezeka na kufikia 17 na hivi karibuni akakamatwa na mwenyekiti wa
Kijiji hicho Willy Joseph na kufikia watu 18 waliofikishwa mahakamani ambapo
hali hiyo imekuwa ikiwafanya kushindwa kufanya shuhuli zao za kimaendeo badara
yake wana wamekuwa wakihudhuria keshi hizo mahakamani na polisi.
Alisema kati ya mwaka 2012/15 tayari Chedego alishawapeleka
wazungu wawili katika eneo hilo kwa nia ya kuwaonyesha kama panafaa kwa kilimo
cha zabibu hali ambayo inaashiria kuwa tayari mashamba yao yameshauzwa kwa
wazungu hao.
“Wajukuu zangu tumepata shida sana mpaka kufikia sasa maana
tunaona kama vile serikali nzima kaiweka mfukoni mwake, hivi kweli mtoto
aliyezaliwa tunamuona kupata hivyo vihela anataka kutukalia vichwani na hivi
huwa tunapata taabu sana kwa sababu wakati mwingine hujifanya kama siyo Mgogo
maana hata huko polisi na mahakamani mwenzetu anaongeaga kizungu hata Kiswahili
hataki hali inayowafanya hata baadhi ya polisi kumuogopa,
Na hao wazungu anaokujaga nao na kwenda kuwaonyesha mashamba yetu kwa sasa hatutakubali
watakapokuja tutawafukuza hatatakubali kuona mashamba ambayo tunayategemea kwa
chakula cha familia zetu mtu mmoja aje kutunyang’anya na kuyauza kwa ajili ya tama
zake”, alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Hicho Willy Joseph
alisema Tayari kijijini hapo kuna viashiria vya uvunjifu wa amani kutokana na
wakazi wengi kutopendezwa na kitendi hicho cha ndugu zao kutishiwa Maisha na
mara nyingi kukamatwa na kufikishwa polisi na mahakamani kwa visingizio
mbalimbali ikiwemo kuvamia shamba lake, kumtishia na mengineyo huku
akiwachonganisha na polisi kuwa wakazi hao wanaongoza kwa fujo huku wakiwakataa
kufika kijijini hapo.
Aliongeza kuwa hata
yeye anashangazwa na kitendo cha kukamatwa kwake akidaiwa kuongoza fujo
kijijini hapo, ambapo aliitaka serikali kupitia vyombo vyake kufanya uchunguzi
wa kina kuhusu mgogoro huo ambao ulianza kufukuta miaka 4 iliyopita ili kuwasaidia
wakazi hao waweze kuishi na kulima kwa amani katika katika mashamba waliachiwa
na Mababu na Bibi zao.
Nae Diwani wa Kata ya Nghon’oha Philip Namga alisema kuwa
Mgogoro huo ameukuta ni wa Muda mrefu sasa lakini hawezi kuuzungumzia kwa kuwa
shauri hilo lipo mahakama ya Wilaya lakini kwa sasa anamsubiri Mbunge wa Jimbo
la Dodoma Mjini Anthon Mavunde ambaye kwa sasa Yupo jijini Dar es Laam kwa shuhuri
za kiserikali ili afikishie Taarifa hiyo ili ajue jinsi ya kuwasaidia wapiga
kura wake.
Hata hivyo Gazeti hili lilishuhudia uhalibifu mkubwa wa
kukatwa kwa mazao mbalimbali yakiwemo mahindi, Alizeti na mtama yakiwa yamefyekwa
katika moja ya shamba kijijini hapo na watu wasiyojulikana, ambapo wadadisi wa
mambo wanasema kuwa inawezekana kuwa ni ulipaji kisasi kutokana na hilo kuwa tukio la tatu
katika mashamba tofauti.
Bado juhudi za kumapata Chedego ili aweze kutoa ufafanuazi
wa Tuhuma dhidi yake zinaendelea kutokana na kutokuwepo kijijini hapo wakati
waandishi walipofanya ziara kijijini hapo.
mhariri:Denis J Kazenzele
feb/18/2016 Alhamis
No comments
Post a Comment