Na Denis Kazenzele
Unapozungumzia Valentine day unazungumzia siku muhimu sana hasa kwa kina dada na watu wanaoijua zaidi starehe na furaha hasa kwa siku tengwa kwa matukio yaletayo furaha katika nafsi ya mtu fulani.
unajiskiaje unapokutana na rafiki yako hasa binti anakwambia chakula anachokipendelea zaidi ni Ugali na Mrenda?, bila shaka wewe kama mwanaume utajiuliza huyu vipi? lakini ni jambo la kawaida sana kwa binti huyu aitwaye Peris John mtangazaji wa kituo cha redio cha Rasi Fm Radio cha mkoani Dodoma ambaye yeye licha ya kupenda mambo mengi na mengine kuyachukia ametokea kupendelea saana ugali na mrenda licha ya kwamba Chips kyuku,na wali njegere ni vyakula ambavyo mara moja moja humpa furaha hasa kwa mlo rasmi.
pia kutokana na Siku hii ya Valentine Nimekutana nae na kufanya nae mahojiano nimepata kufahamu mengi kutoka kwa mwana dada huyu na ukiachana na vyakula pia kuna masuala ya mavazi, yeye anapendelea sana suruari za Jinsi na blauzi laini .
Kama ujuavyo katika huu ulimwengu kuna tabia zinazokera zifanywazo na wanaadamu, nae kama binadamu kuna tabia zinazomkera, tabia hizo ni kama vile...Uongo,Unafki na majivuno pia hakusahau jambo la dharau {kumdharau}.
jambo zuri {neno zuri} analotamani kuambiwa na wake wa karibu ni neno {nakupenda} anadai neno hilo humwingia sawa sawa katika nafsi yake nakujiona wa thamani zaidi kwa {..........}wake.
pia anasema anapenda Music wa ndani kidooogo lakini wa huko nje sana tu {r&b}, pia katika michezo yupo sana katika mchezowa football na ni shabiki wa manchester united kwa upande wa england lakini akiishabikia Fc barcelona kama timu inayocheza mpira anaoupenda yeye na mchezaji anayempenda katika klabu ya manchester united ni Wayne Rooney wakati Mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Christiano Ronaldo ndiye anayevutiwa naye zaidi.
lakini Peria anapenda zaidi zawadi kutoka kwa mpenzi wake na wakati mwingine awapo huko kwao Tanga hupendelea zaidi kutebelea maeneo ya beach na sehemu tulivu..
anaitwa Peris John {Kidawa} mtangazaji mahiri zaidi wa vipindi vya Mahaba Mkoani Dodoma ikiwa unahitaji dawa anakwambia sikiliza kipindi cha Golden Breeze kuanzia mida ya saa nne kamili usiku hadi saa sita usiku kila siku isipokuwa jumamosi pekee....kupitia 103.7 Rasi Fm Radio.....
No comments
Post a Comment