MARCH 29/TUESDAY
Mwanamume huyo alidai kwamba alikuwa na mkanda wa kujilipua na kumwamuru
rubani wa ndege hiyo kuielekeza Cyprus au Uturuki.
Ndege hiyo, iliyokuwa safarini kutoka Alexandria hadi mjini Cairo,
mwishowe ilitua uwanja wa Larnaca nchini Cyprus.
Abiria karibu wote walikuwa wamefanikiwa kuondoka kutoka
kwenye ndege hiyo.
Ripoti zinasema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir anataka kuongea na
mkewe walietengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea
katika uwanja huo wa ndege.
Rais wa Cyprus Nicos
Anastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio hilo la utekaji nyara
halikuwa la kigaidi.
Akijibu maswali ya waandishi iwapo mtekaji huyo alishinikizwa na
mapenzi, alicheka na kusema, ''kila mara kuna mwanamke anayehusishwa''.
Shirika la habari la Cyprus CYBC linasema kuwa mtekaji huyo huenda
alikuwa na malengo yake ya kibinafsi, mtekaji huyo alikuwa na mkewe
waliyetengana nchini Cyprus.
Walioshuhudia wanasema kuwa mtekaji huyo alirusha barua katika uwanja
huo wa ndege ilioandikwa Kiarabu akiomba ipelekwe kwa mwanamke huyo.
Silaha hizo ni pamoja na mamia ya bunduki pamoja na silaha za kupambana
na vifaru.
Hatua hiyo inajiri wiki kadhaa baada ya wanamaji wa Australia kukamata
silaha nyingi zilizokuwa zikielekea Somalia.
Meli hiyo ilionekana na ndege za wanamaji wa Ufaransa ambayo ni mojawapo
wa vikosi vya kimataifa vinavyopiga doria katika bahari Hindi.
Vikosi hivyo vya
Ufaransa vilikamata silaha hizo chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa kuzuia
silaha kutowafikia wapiganaji wa wa al-shabab.
Muungano huo wa wanamaji umepongeza kukamatwa kwa silaha hizo kama
mafanikio makubwa ijapokuwa haujatoa habari zozote kuhusu wale wanaosafirisha
silaha hizo.
ITALIA
Meya wa mji wa
Ostana, ulioko Kaskazini mwa Italia ambayo iko katika maeneo ya milima ya
Piedmont aliwaongoza wenyeji kusherehekea ndoto yao kukamilika kwa kuzaliwa kwa
kizazi kipya.
Ostana imeshudia
kupungua kwa idadi ya wenyeji wake katika karne iliyopita kwa hivyo kuzaliwa
kwa ''Pablo'' katika hospitalini moja ya Turin imeongezea idadi ya wenyeji
kufikia 85.
Jarida la La Stampa linasema
japo wanasheherekea sio wote wanaoishi mjini humo.
Meya Giacomo
Lombardo anasema kuwa miaka ya nyuma Ostana ilikuwa na wenyeji 1,000 lakini
idadi hiyo ya watu imekuwa ikipungua kila kukicha hadi kufikia 85 sasa.
''Mara ya mwisho
mtoto kuzaliwa hapo ni mwaka 1987''
amesema Kati ya mwaka wa 1975 -1976 watoto 17
walizaliwa katika mji huo.
Kwa sasa wenyeji
wa mji huo wa Ostana wameanza kuweka mikakati ya kuimarisha idadi ya watoto
wanaozaliwa kwa kuunda nafasi mpya za kazi.
Wazazi wa Pablo,
Silvia na Jose walikuwa wamepanga kuondoka Italia kabla ya wenyeji kuwapa
nafasi ya kuwa meneja wa uhifadhi wa misitu Ostana.
Kwa sasa
wanapiga msasa sheria itakayowaruhusu wenyeji wasilipe kodi mbali na kutoa
nyumba za bure kwa wenyeji wanaotafuta kazi.
SOMALIA
Silaha hizo ni pamoja na mamia ya bunduki pamoja na silaha za kupambana
na vifaru.
Hatua hiyo inajiri wiki kadhaa baada ya wanamaji wa Australia kukamata
silaha nyingi zilizokuwa zikielekea Somalia.
Meli hiyo ilionekana na ndege za wanamaji wa Ufaransa ambayo ni mojawapo
wa vikosi vya kimataifa vinavyopiga doria katika bahari Hindi.
Vikosi hivyo
vya Ufaransa vilikamata silaha hizo chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa
kuzuia silaha kutowafikia wapiganaji wa wa al-shabab.
Muungano huo wa wanamaji umepongeza kukamatwa kwa silaha hizo kama
mafanikio makubwa ijapokuwa haujatoa habari zozote kuhusu wale wanaosafirisha
silaha hizo.
NIGER
Wapinzani nchini
Niger wametangaza azma yao kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Mahamadou
Issoufou wa nchi hiyo.
Chama kikuu cha
upinzani ambacho pia kimetangaza kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita
nchini humo, kimeyasema hayo baada ya kukutana na Brigi Rafini, Waziri Mkuu wa
nchi hiyo.
Katika taarifa
yake, chama hicho kinachoongozwa na Hama Amadou, kimetangaza utayarifu wake kwa
ajili ya kuzungumza na rais huyo aliyeibuka mshindi katika uchaguzi huo.
Aidha chama hicho
kimetaka mazungumzo hayo yawe ya kweli na jadi kwa ajili ya kumaliza mgogoro wa
kisiasa ambao unaendelea nchini Niger tangu kujiri uchaguzi mkuu uliopita.
Rais Mahamadou
Issoufou aliibuka mshindi baada ya kupata asilimia 94/92 ya kura katika
uchaguzi wa duru ya pili uliofanyika tarehe 20 mwezi Machi mwaka huu.
Chama kikuu hicho
cha upinzani kiliutaja uchaguzi huo kuwa wa kimaonyesho suala ambalo lilisababisha
chama hicho kuususia.
No comments
Post a Comment