VINARA wa Ligi Kuu England Leicester City wamezidi kupaa juu zaidi kileleni baada Jana kuifunga Watford Bao 1-0 wakicheza Ugenini.
Bao hilo pekee lilifungwa katika Dakika ya 56 na Riyad Mahrez.
Sasa Leicester wanaongoza Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Tottenham ambao Jana walitoka Sare 2-2 na Arsenal Uwanjani White Hart Lane.
Arsenal wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 8 nyuma ya Leicester.
Nao Man City wameicharaza Timu ya Mkian Aston Villa Bao 4-0 huku Bao zote zikifungwa Kipindi cha Pili na Yaya Toure, Sergio Aguero, Bao 2, na Raheem Sterling.
Nao Mabingwa Watetezi Chelsea, wakicheza kwao Stamford Bridge, walitoka Sare 1-1.
Bao za Mechi hiyo zilifungwa na Bertrand Traore Dakuka ya 39 kwa Chelsea na Mame Biram Diouf kkusawazisha Dakika ya 83 kwa Stoke.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
Jumamosi Machi 5
Tottenham Hotspur 2 Arsenal 2
Southampton 1 Sunderland 1
Man City 4 Aston Villa 0
Chelsea 1 Stoke City 1
Everton v West Ham
Swansea City 1 Norwich City 0
Newcastle 1 Bournemouth 3
Watford 0 Leicester City 1
Jumapili Machi 6
1630 Crystal Palace v Liverpool
1900 West Brom v Man United
No comments
Post a Comment