Baada ya usiku wa March 1 kuchezwa
michezo mitano ya Ligi Kuu Uingereza, usiku wa March 2 iliendelea tena
michezo ya Ligi Kuu Uingereza, kwa mechi tano nyingine kupigwa katika
viwanja mbalimbali Uingereza.
Baadhi ya michezo ya Ligi Kuu Uingereza
iliyochezwa usiku wa March 2 ni mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Man
City, Arsenal dhidi ya Swansea City na Man United dhidi ya Watford,
mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Man City ndio ulikuwa unatazamwa kwa
kiasi kikubwa.
Man City ambao walikuwa ugenini katika uwanja wa Anfield, walikubali kipigo cha goli 3-0, Magoli ya Adam
Lallana dakika ya 34, James Milner dakika ya 31 na Roberto Firmino
dakika ya 57 yalitosha kuimaliza Man City ndani ya Anfield.
Kipigo hicho kimewafanya Man City wabaki
nafasi ya nne wakiwa na point 47 katika michezo ya 28, wakati Liverpool
wakiwa nafasi ya nane katika Ligi na wametimiza jumla ya point 41 baada
ya ushindi huo wakiwa michezo sawa na Man City.
Matoke ya mechi za Ligi Kuu Uingereza March 2
-
Arsenal 1 – 2 Swansea City
-
Stoke City 1 – 0 Newcastle United
-
West Ham United 1 – 0 Tottenham Hotspur
-
Liverpool 3 – 0 Manchester City
-
Manchester United 1 – 0 Watford
Arsenal 1 – 2 Swansea City
Stoke City 1 – 0 Newcastle United
- West Ham United 1 – 0 Tottenham HotspurManchester United 1 – 0 Watford
No comments
Post a Comment