Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini vijana wake walicheza vyema uwanjani Nou Camp licha ya kulazwa 3-1 na Barcelona Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Arsenal walilazwa kupitia mabao ya Neymar, Luis Suarez na Messi. Bao lao la kufutia machozi lilifungwa na Mohamed Elneny.
Arsenal hawajafika hatua ya robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tangu 2010.
"Nafikiri tulicheza vyema, ulikuwa mchezo mzuri kati ya timu mbili nzuri. Tumeondolewa kwa masikitiko lakini wana ustadi wa hali ya juu hasa katika safu ya mashambulizi na ukifanya kosa kidogo tu safu yako ya ulinzi wanaweza kukuadhibu,” alisema Wenger baada ya mechi.
"Wakati muhimu katika mchezo huo ni mambo yalipokuwa 1-1 kwa sababu nilidhani walikuwa wanayumbayumba kiasi. Kama tungefunga bao la pili wakati huo badi mambo yangekuwa tofauti labda. Lakini hatukuweza."Katika michezo yote miwili, ukiangalia nafasi ambazo tuliunda, zilikuwa nyingi. Inauma kuondolewa kwenye michuano lakini tulicheza vyema sana dhidi ya timu ambayo labda ndiyo bora zaidi Ulaya.”
Arsenal walilazwa 2-0 mechi ya mkondo wa kwanza uwanjani Emirates, mabao yote yakifungwa na Lionel Messi.
Katika mwingine Bayern Munich imechomoza na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Juventus ya Italia.
Mabao ya Bayern yamefungwa na Lewandowski, Thomas Muller, Thiago Alcantara na Kingsley Coman, huku magoli ya Juventus ya kifungwa na Paul Pogba, na Juan Cuadrado.
Kwa matokeo hayo Bayern imeshinda jumla ya bao 6-4 kufuatia sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa awali.
No comments
Post a Comment