Julius Malema |
Mtuhumiwa huyo hakujibu maswali yote aliyoulizwa na jaji.
Anashtakiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari na ubakaji alipokuwa mkuu
wa wilaya ya Nyakizu kusini mwa Rwanda mwaka 1994.
Bw Ntaganzwa amefikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali wa askari
polisi pia kukiwa na watu wengi waliokuja kuhudhuria kesi wakiwa ni manusura wa
mauaji ya kimbari kutoka wilaya ya Nyakizu.
Mwendesha mashtaka amemfunguliwa mashtaka matano yakiwemo mauaji ya
kimbari, kuhamasisha genge la Wahutu kutekeleza mauaji hayo na ubakaji.
Ameiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alitekeleza makosa hayo katika sehemu
mbali mbali za wilaya ya Nyakizu, kusini mwa Rwanda.
Alipoulizwa kuhusu
hoja ya mwendesha mashtaka, mshtakiwa ameamua kukaa kimya na hakutoa jibu
lolote.
Wakili wake amesema kuwa hana lolote ya kuiambia mahakama hii ya mwanzo
akisisitiza haina mamlaka ya kuendesha kesi hiyo.
Kesi dhidi ya Bw
Ntaganzwa, sawa na za watuhumiwa wengine wa mauaji ya kimbari waliokuwa
wanasakwa na mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda ICTR, inasikizwa na
kitengo maalumu cha mahakama kuu nchini Rwanda baada ya kufungwa kwa ICTR
mwishoni mwa mwaka jana.
Jaji alisema kesi ilioanza leo ni ya mwanzo na kusudi lake ni kutafuta
kifungo cha muda kabla ya kesi yenyewe kuanza kusikilizwa kwa undani wake.
Bw Ntaganzwa alikabidhiwa Rwanda wiki mbili
zilizopita kutoka DR
Congo.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
TECHNOLOGY KUHUSU KUNDI LA TALIBAN
Programu inayotumiwa katika simu za Android Alemarah, iliyoundwa
na kundi la wapiganaji wa Taliban imeondolewa kwenye soko la programu la
Google, Play Store.
App hiyo
iliyozinduliwa tarehe 1 April, miongoni mwa mengine, ilikuwa na taarifa rasmi
na video kutoka kwa kundi hilo la Kiislamu kwa lugha ya Pashto.
Kundi hilo limesema kumetokea “hitilafu za kiufundi” baada ya app hiyo
kutoweka.
Hata hivyo imefahamika kwamba app hiyo imeondolewa kwa sababu inakiuka
kanuni na sera za Google zinazokataa uchochezi.
App hiyo iligunduliwa na shirika la Marekani la Site Intel Group
linalofuatilia shughuli za makundi ya kijihadi.
Google imekataa kuzungumzia app hiyo binafsi lakini ikasema kupitia
taarifa kuwa: “Sera zetu zimeundwa kuridhisha wateja wetu na watu
wanaotengeneza app. Ndio maana huwa twatoa apps zinazokiuka sera hizi kutoka
kwenye Google Play."
Msemaji wa kundi la Taliban alikuwa ameambia Bloomberg kwamba app hiyo
ilikuwa “sehemu ya juhudi za kiteknolojia za kufikia watu zaidi duniani.”
Serikali ya taifa hilo la Magharibi mwa Afrika inasema kuwa kutokana na
mafunzo ya dini ya kiislamu wamekubalika kuwapokea walibya hao 2 kwa mujibu wa
waziri wa maswala ya kigeni wa nchi hiyo.
Wafungwa hao 2 walikuwa wanatumikia kifungo cha miaka 14 jela bila
kufunguliwa mashtaka yeyote.
Kauli hiyo inafuatia uamuzi wa serikali ya rais Barack Obama ya kufunga
jela hiyo ya kisiwa cha Guantanamo Bay.
Rais huyo wa Marekani
aliahidi kufunga kituo hicho miaka 7 iliyopita.
Mataifa machache yamekubali kuwapokea wafungwa wa Guantanamo Bay
yakiwemo baadhi ya mataifa ya kiafrika kama Uganda, Ghana na Cape Verde.
Waziri Emmanuel Ibe Kachikwu ameelezea ''uchungu'' uliosababishwa na
upungufu huo wa mafuta ya magari.
Bw Kachikwu ameahidi kumaliza kabisa upungufu wa aina hiyo kote nchini.
Aidha amesema kuwa serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwepo
kwa mafuta nchini humo.
Katika majuma kadhaa
yaliyopita foleni ndefu ya magari pikipiki na hata lori imeshuhudiwa kwenye
vituo vya kuuzia bidhaa hiyo adimu.
Wenye magari wanasema kuwa wakati mwengine wanalazimika kupiga foleni
kwa masaa mengi mno .
Wengi wanajiuliza itakuwaje kuwa Nigeria ndilo taifa linalozalisha idadi
kubwa zaidi ya mafuta barani Afrika ilhali hata nyumbani hawana mafuta ya
magari?
Wasilolijua ni kuwa
Nigeria haina mtambo wa kusafisha mafuta na hivyo lazima iagize kutoka nje
mafuta ya matumizi yake ya nyumbani.
Wauzaji mafuta wanasema kuwa kuna utashi mkubwa wa dola za Marekani
wanazohitaji kununua mafuta.
Lakini kuna madereva wanaoshuku utashi huo wakidai kuwa huenda ni njama
ya wauzaji mafuta kuongeza bei ya bidhaa hiyo
Kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter chama chake cha EFF kinasema
kuwa Kamanda wao aliviziwa na polis ambapo takriban magari kumi ya polisi ambao
wote walimelekezea mtutu wa bunduki baada ya kulizuia gari lake katika makutano
ya barabara ya Grayston .
Taarifa hiyo inasema
kuwa hali hiyo inaonesha wazi kuwa serikali ambayo sasa imekabwa koo na tuhuma
za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa mali ya umma imeanza kutumia
mbinu hiyo na kutumia nguvu kinyume cha sheria.
Msemaji wa polisi amesema
kuwa hakufahamu lolote kuhusu tukio hilo.
EFF na bwana Malema wanaongoza kampeini ya kumng'oa rais Zuma madarakani
kufuatia utepetevu na ubadhirifu wa mali ya umma.
Chama hicho kilipata uungwaji mkono juma lililopita mahakama ya juu
zaidi nchini humo ilipompata Zuma na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka yake na
ubadhirifu wa fedha kuhusiana na ukarabati wa makazi yake ya Nkandla.
Zuma akekanusha kufanya makosa yeyote ila amekubali kurejesha fedha
zilizotumika katika ukarabati huo ilokiuka sheria za nchi.
No comments
Post a Comment