NA.Ezekiel Kamanga,Chunya.
Wakazi
wa kijiji cha Ifumbo wilayani Chunya mkoani Mbeya wameunda kamati ya
ufuatiliaji wa uuzwaji wa trekta la kijiji hicho lililouzwa na uongozi
wa halmashauri ya kijiji kwa shilingi milioni tano bila kushilikisha
wananchi.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti katika mkutano hadhara wa kijiji wakati wakisomewa
mapato na matumizi ya kijiji wakazi hao walisema wanataka kurudishiwa
trekta lao kwani hawajaridhika na bei hiyo waliuza ukilinganisha na
thamani ya trekta.
Waliendelea
kueleza kuwa kama walipata mteja kwa bei hiyo wangeitisha mkutano wa
hadhara ili wananchi wakubaliane na bei hiyo aliyoitaja mteja huyo au
laa,lakini badala yake wao kama uongozi wa kijiji wakachukua maamuzi
bila kulileta kwa wananchi kitu walichopinga vikali na kutaka trekta yao
irudishwe kijijini halo.
Akizungumzia
suala hilo mwenyekiti wa kijiji hicho cha ifumbo Lyashi Mwambyalo na
kaimu mtendaji Emily Rajabu walisema kuwa wao waliamua kuuza bei hiyo
kutokana na trekta hiyo kuonekana kuwa ni chakavu na vifaa vingi
vimepotea na kwamba wananchi walivyowambia liuzwe hawakuta bei ya kuuza
hilo trekta.
Kwa
upande wake diwani wa kata hiyo Michael Zanzi akizungumzia suala hilo
alisema kuwa yeye kama mwakilishi wa wananchi akizungumzia uuzaji wa
trekta alisema kuwa yeye licha ya kujua kuwa wananchi walitoa maoni ya
kuuzwa kwa trekta hilo lakini hakuweza kuhusishwa na halmashauri ya
kijiji katika mchakato mzima badala yake aliitwa siku ambayo mteja
amefika na wamekubaliana bei wakiwa wanaendelea na kikao wakiwa wametaja
hiyo bei.
Zanzi
aliendelea kueleza kuwa yeye hakukubaliana kabisa na kuuzwa kwa trekta
hiyo kwa bei hiyo ya shilingi 5 miloni na akashauri halmashauri ya
kijiji kite mkutano wa kijiji ili wananchi lakini akashangaa viongozi wa
kijiji wamechukua fedha bila kuita mkutano wa hadhara na kuleza kuwa
wananchi wana haki ya kudai trekta hilo kwasababu hawezekani trekta
kuuzwa sh.5 milioni.
No comments
Post a Comment