Na. Ezekiel Kamanga,Chunya.
Wanakijiji
wa kijiji cha Ifumbo wilayani Chunya mkoani Mbeya wanawashikilia wazee
wa mila(machifu) kwa tuhuma ya kujihusisha na imani za kishirikina na
kutupia majini shuleni na kusababisha wanafunzi kuzimia kwa kile
kinachodaiwa uongozi wa shule ya hauwaaliki kwenye mahafali na
kuwaheshimu kama machifu wa kijiji.
Wakizungumza
wananchi wa kijiji hicho akiwemo Braisoni Mwansimba walisema kuwa
tatizo hilo la kuzimia kwa wanafunzi katika shule hilo lilianza tangu
mwaka jana mwezi wa nne na lilianza kwa mtoto mmoja hadi kufikia 20 kwa
siku hali iliwashitua wakazi wote kijijini hapo na kwamba
wanafunzi wanapozimia huwa wanaweweseka huku wakitembelea
tumbo mithili ya nyoka.
Waliendelea
kueleza kuwa kutokana na tatizo hilo kuzidi halmashauri ya kijiji na
wananchi wote waliamua kuwaita wazee hao ili kutatua tatizo hilo lakini
wazee hao walisema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na kwamba
uongozi wa shule na kijiji hicho kutowaalika katika pindi mahafali
yanapofanyika shuleni halo na shughuli zingine za kijiji na ndio chanzo
cha kufanya hivyo shuleni halo.
Akizungumzia
suala hilo mkuu wa shule hiyo Malema alisema kuwa kutokana na kuzidi
kwa tatizo hilo uongozi wa kijiji uliamua kutafuta ufumbuzi kwa kijiji
jirani cha ikukwa na kubaini kuwa wazee wa mila ndio chanzo na ndipo
walipoamua kupeleka wagaga wa jadi kutoka mbozi na ikukwa ili wazee hao
wanyweshe dawa ili kuwatoa uchawi na waliponyweshwa hiyo dawa tatizo
hilo lilizidi hali iliyowalazimu kuwaita tena.
Aliendelea
kueleza kuwa mbali na tatizo hilo kudumu kwa muda mrefu kama mwaka sasa
mwenyekiti wa kijiji alipokuwa akiambiawa tatizo bado aliendelea
kufumbia macho kwa madai kwamba atakapogombea tena 2020 ataangushwa hadi
diwani alipoingilia kati mara baada ya uchaguzi wa octoba 2015.
Aidha
diwani wa kata hiyo Michael Zanzi alifafanua kuwa kutokana na juhudi
hizo za kutafuta ufumbuzi katika vijiji jirani tatizo hilo limeweza
kupungua kwa kiasi kutoka wanafuzi 20 hadi kufikia mtoto mmoja au wawili
kwa siku kwani walifanikisha kuwanyweshwa kabwela wazee waliokuwa
wakituhumiwa na kutawapatia dawa za kienyeji wanafunzi wa shule huyo na
kwamba siku ya jumapili watakaa na wazee hao ili kuhakikisha tatizo hilo
linapungua kama si kuisha kabisa.
No comments
Post a Comment