Watu watatu akiwemo raia wa Kenya wanashikiliwa na
jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina
ya Mirungi na Bangi kilo 54 na misokoto ya Bangi 4,500 ikisafirishwa kutoka
nchini Kenya kwenda mkoani Arusha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Bw.Wilbrod
Mutafungwa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo ya njia panda Himo
wilaya ya Moshi na Sanya juu wilaya ya Siha wakiwa wameficha madawa hayo ya
kulevya kwenye miili yao kuanzia maeneo ya tumboni hadi miguuni.
Amewataja waliokamatwa ni Vitalis Victor mfanyabiashara
mkoani Arusha, Naftal Mvoyi mkazi wa Voi nchini Kenya, Maulid Maulis mkazi wa
Arusha ambao walikuwa wakisafirisha Mirungi kilo 44 kwa kutumia magazeti na
gundi ya karatasi na kisha kuifunika kwenye nguo walizokuwa wamevaa wakitokea
nchini Kenya kuelekea jiji la Arusha.
ITV imefanikiwa kuzungumza na baadhi ya vijana
wanaojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya katika manispaa ya Moshi na
kueleza kwamba changamoto kubwa inayowabaili ni ukosefu wa ajira hali
inayowasababisha baadhi yao kujihusisha na matukio ya uhalifu.
Matumizi ya madawa ya kulevya yameathiri vijana
wengi kiafya kutokana na baadhi yao kushindwa kufanya shughuli za maendeleo na
hivyo kulazimika kujihusisha na matukio ya wizi katika maeneo mbalimbali hapa
nchini.
No comments
Post a Comment