kumbukumbu ya picha ya Nyoso akifanya tukio la udhalilishaji dhidi ya Elius Maguri msimu uliopita wakati Maguri akicheza kwenye klabu ya Simba SC na tukio hilo hilo amelifany akatika mechi dhidi ya Azam fc jana
Mchezaji na nahodha wa timu ya
Mbeya City Juma Nyoso ameendelea kufanya vitendo ambavyo si vya
kiungwana na vinavyohitaji kupingwa kwa nguvu zote kwenye soka si la
Tanzania pekee bali duniani kote ambako mchezo huu unachezwa.
Nyoso amemfanyia kitendo cha
udhalilishaji mchezaji na nahodha wa Azam FC John Bocco ‘Adebayo’ wakati
wa mchezo wa timu ya Azam FC dhidi ya Mbeya City uliochezwa kwenye
uwanja wa Azam Complex, Chamazi ambapo Azam FC waliiibuka na ushindi wa
goli 2-1.
Kitendo kilichofanywa na Juma
Nyoso ni cha kulaaniwa na kupigwa vita kwasababu kinaharibu maana halisi
ya mchezo wa soka ambao ni wa kistaarabu unaochezwa na waungwana
wapenda amani lakini kwa beki huyu wa Mbeya City haiko hivyo.
Msimu uliopita Nyoso alimfanyia
kitendo kama alichokifanya leo kwa John Bocco aliyekuwa mshambuliaji wa
Simba kwa wakati huo Elius Maguri ambaye kwa sasa anakipiga Stand United
ya Shinyanga. Mazingira ya matukio hayo mawili yanafanana kwa asilimia
nyingi.
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi amethibitisha hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mchezaji aliyefanya kitendo hicho, Malinzi amethibitisha hilo kupitia account yake rasmi ya twitter. Lakini hii sio mara ya kwanza kwa beki na nahodha wa Mbeya City Juma Nyoso kufanya kitendo hicho, alishawahi kumfanyia Elias Maguli na kupewa adhabu ya kufungiwa mechi nane mwanzo mwa mwaka 2015.
haya ndio maneno aliyoyaandika mheshimiwa Rais wa Tff
No comments
Post a Comment