habari zaidi
Buzwagi
imeanzisha mkakati wa kukuza na kuboresha hali ya utendaji kazi kwa
wafanyakazi wake kwa kuanzisha utaratibu wa kuwakutanisha wafanyakazi wa
mgodi huo na familia zao mara moja kwa mwaka katika siku maalumu ya
familia ambayo hutoa fursa kwa familia za wafanyakazi wa mgodi huo
kuweza kujionea namna ambavyo shughuli za uchimbaji wa madini hufanyika
na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa kampuni kwa ujumla.
Mwaka
huu wafanyakazi wa kampuni hiyo wamepata fursa ya kukutana na kujionea
shughuli mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika mgodi hapo. Pamoja na
mambo mengine wafanyakazi hao pia walipata fursa ya kutembelea eneo
ambapo shughuli za uchimbaji zinafanyika.
Sherehe
hizo zilihudhuliwa na Afisa mkuu wa masuala ya uendeshaji Michelle
Ash, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulur-Graham Crew na meneja mkuu wa
masuala ya ufanisi wa kampuni Janet Ruben pamoja na meneja mahusiano na
mawasiliano wa Acacia Nector Foya, pamoja na viongozi mbalimbali wa
serikali..
No comments
Post a Comment