Mshambuliaji Alexis Sanchez wa Arsenal amerejea katika ubora wake baada ya weekend hii kufunga magoli matatu ‘hat-trick’ katika mchezo wa ligi kuu England Arsenal ikiifunga Leicester kwa jumla ya mabao 5-2.
Hat-trick hii imemfanya Sanchez
aweke rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat-trick katika ligi kuu
tatu tofauti duniani, Serie A, La Liga na EPL .
Hat-trick yake ya kwanza ilikuja
akiwa anaichezea Udenise ya Italia wakiizamisha Palermo mabao 7-0 katika
mchezo wa ligi kuu soka nchini Italia 2011.
Sanchez alisajiliwa Barcelona
akitokea Udenise ya Italia kwa pauni 23m na kisha kufanikiwa kupiga
hat-trick nyingine ya pili nchini Hispania Barcelona wakiwafunga Elche
mabao 4-0.
Magoli matatu ya Sanchez
yaliisaidia Arsenal kuifunga Leicester ambayo ilikua haijafungwa hata
mchezo mmoja tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu.
Huku mchezaji mwenza
wa Arsenal, Theo Walcott akimwaga sifa kwa Sanchez kuwa ni bora zaidi
kikosini.

No comments
Post a Comment