Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhukumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.
Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.
Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh 800,000/- ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.
Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.
"Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema.
No comments
Post a Comment