Choo cha mwalimu mkuu shule ya Msingi Mdeke Kilolo ************************************************************* |
MBUNGE wa jimbo la Kilolo
mkoani Iringa Venance Mwamoto amechangia zaidi ya Tsh milioni 20
kwa ajili ya kukamilisha miradi mbaali mbali
ya kimaendeleo ikiwemo ya ujenzi wa vyoo
vya wanafunzi ,madarasa ,nyumba za walimu na Zahanati
katika jimboni hilo huku akiwataka viongozi wa serikali
za vijiji na kata kuhakikisha wanakamilisha
ujenzi huo kwa wakati na ubora .
Pamoja na kuwataka viongozi
hao kusimamia ujenzi huo amesema atachukua hatua
kali kwa kiongozi yeyote wa serikali ya kijiji
ama kata ambaye atatafuna fedha hizo za
ukamilishaji wa miradi hiyo ya kimaendeleo jimboni humo.
Mbunge huyo aliyasema
hayo jana wakati alipofanya ziara ukaguzi
wa miradi 9 inayoendelea kwa nguvu za
wananchi na Halmashauri ya wilaya ya Kilolo
na kueleza kuvutiwa na miradi hiyo
japo kunahitajika msukumo wa haraka katika
umaliziaji wa miradi hiyo hasa ile ya vyoo vya
wanafunzi ili kuwawezesha wanafunzi hao pindi shule
zinapofunguliwa kuwa na vyoo bora.
Alisema kutokana na hali ya hewa
kuwa mbaya kwa mvua kuchelewa kunyesha katika
maeneo mbali mbali ya wilaya ya Kilolo tofauti na miaka
mingine ameona ni vema kuwapunguzia makali ya michango
wananchi wake na badala yake sehemu ya michango
ambayo walipaswa kuchangia ili kukamilisha miradi
hiyo kuibeba yeye kupitia mfuko wa jimbo
kwa kuchangia fedha hizo.
Kwani alisema ni rahisi kwa
wananchi kuchangia nguvu zao kwa kushirikia
katika ujenzi huo wa miradi hiyo kuliko kushiriki
kutoa fedha jambo ambalo kwa wananchi hao ni sawa
na kuwatesa kutokana na wengi wao waliuwa
wakiishi kwa kutegemea kilimo na hadi sasa matumaini
ya kupata fedha kwa njia ya kilimo yametoweka baada ya
mvua kushindwa kunyesha.
“Ninawaombeni sana wananchi wangu
kwa sasa ninyi mshiriki zaidi
katika maendeleo kwa kuchangia nguvu
zenu na mimi niwaunge mkono kwa kuchangia fedha
ili kuifanya miradi hii ikamilike kwa wakati”
Hata hivyo alisema kuna
baadhi ya maeneo wananchi wanachangamoto kubwa
ya barabara hasa zile
zilizopo chini ya Halmashauri kuwa barabara hizo
zitafanyiwa matengenezo na ile ya Tanrod kutoka makao makuu ya
wilaya ya Kilolo hadi Ndiwili mpakani mwa jimbo la
Kalenga inaanza kujengwa kwa kiwango cha lami
mapema mwakani na kuwa kuanzia January ujenzi huo
utaanza kwani barabara hiyo ipo
katika ilani ya uchaguzi ya CCM.
Mbunge Mwamoto alisema kuwa kwa suala
la ujenzi wa Zahanati na vituo vya
afya wananchi wamejitahidi kwa maeneo
mbali mbali aliyopita kukagua
ujenzi umefikia hatua nzuri
na kutolea mfano ujenzi wa Zahanati ya Masege ambao
jengo lake bado kuezekwa na nyumba ya
mganga ipo katika hatua ya kuanza
kupandisha kuta kuwa kukamilika kwa Zanahati hiyo
kutawawezesha wananchi hao ambao walikuwa
wakilazimika kufuata matibabu Kibengu na Usokami wilaya
ya Mufindi
wataweza kutibiwa katika Zanahati
hiyo.
Alisema katika ziara yake hiyo
aliyoambatana na wajumbe wa mfuko wa jimbo
kupitia fedha za mfuko wa
jimbo Kijiji cha Mdeke ambako kuna ujenzi wa vyoo vya
wanafunzi amechangia Tsh milioni 1 na kwenye ujenzi wa nyumba
ya mwalimu amechangia Tsh milioni 2 , sekondari ya
Ipeta kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya
wanafunzi amechangia Tsh milioni 2, shule ya Msingi Kidabaga
amechangia Tsh milioni 3 kwa ajili ya vyoo na nyumba ya
mwalimu ,Wangama amechangia Tsh milioni 1 kwa ajili ya
ukarabati wa madarasa ,Kitongoji cha Ifiga amechangia Tsh milioni 1
kwa ajili ya kuanzisha mkondo B wakati ujenzi wa Zahanati
na nyumba ya Mganga Masege amechangia Tsh milioni 5
Mbunge Mwamoto alisema ujenzi
wa kituo cha Afya Ukumbi amechangia Tsh milioni 2
na katika ujenzi huo nguvu za wananchi ni Tsh
milioni 35 na Halmashauri ni Tsh milioni 10 huku
ujenzi wa vyumba vyamadarasa shule ya Msingi
Italula amechangia Tsh milioni 2 hata hivyo alisema
atafanya ziara ya ukaguzi na uchangiaji wa
miradi ya maendeleo katika jimbo zima ili kupitia
mfuko huo wa jimbo miradi yote iweze kupata
mgao huo.
No comments
Post a Comment