Mswada wa sheria mtandao nchini Thailand uliwekwa mezani kujadiliwa takriban wiki kadhaa zilizo pita. Muswada huo ambao ulikua ukingoja kupitishwa kua sheria umepelekea kelele nyingi Nchini humo ambapo wananchi wake walitaka ufanyiwe marekebisho kabla ya kua sheria huku wengine wakiukataa kabisa.
Wana usalama mtandao nchini humo walijaribu kutoa ufafanuzi ambao haukuzaa matunda na hatimae kutaka msaada kutoka kwa wanausalama mtandao wa maeneo mengine.
Wiki mbili zilizo pita wahalifu mtandao Nchini humo walitangaza kushambulia tovuti za serikali ili kushinikiza mamlaka kufanyia kazi marekebisho ya sheria hizo za mtandao ambazo walidai hawakukubaliana nazo – Baadae walianza kushambulia tovuti mbali mbali na kusababisha mtafaruku mkubwa.
Tovuti ya polisi ya nchini humo (Royal Thai Police Office) ni miongoni mwa tovuti zilizo shambuliwa kimtandao ambapo ilidukuliwa na baadae kuangushwa kabisa. Kitu ambacho kilipelekea hasira kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo.
Naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi Mh. Prawit Wongsuwon, alitangaza kukamata washukiwa tisa (9) wa uhalifu huo mtandao pamoja na vifaa vyao huku akiongeza ya kua serikali ya nchi hiyo haita linyamazia tukio hilo na kusema watachukua hatua stahiki kwa kila atakae thibitika na uhalifu huo.
No comments
Post a Comment