St Etienne wamepia stop kuuza ticket za mechi ya Europa dhidi ya Manchester United masaa machache baada ya kuanza kuziuza.
Kufunga huko kumetokana watu wengi kujazana wakitaka kununua hizo ticket licha ya mabadiriko makubwa kwenye bei kama ilivyozoeleka.
Watu wengi wanataka kuona mechi hiyo ambayo itaifanya pia St Etienne ionekane sana duniani kutokana na kucheza na Manchester United. Mashabiki wanataka pia kuona club yao ikicheza dhidi ya mastaa wa EPL.
Kitu kingine kizuri ni pale wanapotaka kumuona mtu na kaka yake wakicheza dhidi ya timu tofauti. Paul Pogba atakuwa anakabwa na kaka yake Florentin Pogba ambae anacheza St Etienne.
Kutokana na kuzuia kuuzwa kwa ticket hizo, St Etienne wamewapa nafasi ya upendeleo mashabiki wenye ticket za msimu mzima (Season ticket holders) nafasi ya kununua ticket hadi nne kila mtu hadi ikifika Dec 23 na wengine wafuatie.
No comments
Post a Comment