Uongozi wa Benchi la Ufundi la Yanga chini ya Kocha Mzambia, George Lwandamina na wachezaji wote wa timu hiyo, hivi karibuni walimuaga aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Mnyarwanda, Mbuyu Twite, kwa kumkabidhi jezi iliyokuwa na saini zao pamoja na picha kubwa.
Twite aliyejiunga na Yanga mwaka 2012, alimaliza mkataba wake hivi karibuni huku uongozi ukishindwa kumuongezea.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema wameamua kumpa zawadi hiyo kama kuthamini mchango wake alioutoa wakati wapo naye.
“Ilikuwa ni zawadi ya kumuaga tu ambayo nimeifanya mwenyewe kwa kumpatia picha yake kubwa iliyowekwa kwenye fremu na jezi ilikuwa na saini za wachezaji wote pamoja na benchi zima la ufundi, kama ishara ya upendo wetu kwake.
“Unajua Twite ameondoka Yanga kwa kuwa mkataba wake ulikuwa umeisha na hakuwa na matatizo na wachezaji wenzake wala benchi la ufundi, sasa kama meneja nimeona ni vyema kama timu tuthamini mchango wake kwa muda wote tuliokuwa naye kwa kumpatia zawadi pamoja na kutamkia mema huko aendako,” alisema Saleh.
No comments
Post a Comment