
Eva Carneiro ambaye anaripotiwa kuondoka rasmi Chelsea anamtuhumu kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho kuwa alimfanyia ubaguzi wa kijinsia wakati akitoka uwanjani kumtibia Eden Hazard, stori kutoka 101greatgoals.com na moroccoworldnews.com zinaripoti kuwa ushaidi tayari umekabidhiwa kwa chama cha soka Uingereza FA, uchunguzi ulifanywa kwa kumtumia mtafsiri wa kireno na kubaini kuwa Mourinho alimfanyia ubaguzi wa kijinsia Eva Carneiro.
Eva Carneiro ambaye toka aingie katika malumbano na kocha huyo wa kireno hajawahi kukaa katika benchi na kuendelea kutoa huduma, Jumanne ya wiki hii alitangaza rasmi kujiuzulu kuendelea kuwa daktari wa Chelsea, kosa alilofanya Mourinho litampelekea kufungiwa mechi tano kwa sababu ya kumtusi Eva Carneiro kwa kutumia lugha ya kireno “filha de puta” ambapo maana yake ni kuwa binti wa mwanamke muhuni.
No comments
Post a Comment