Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » POLISI YAUA MAJAMBAZI HATARI ARUSHA.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

ATU watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi ambao ni raia wa Kenya pamoja na Mtanzania mmoja wameuawa katika mapambano na polisi yaliyotokea eneo la Chekereni mpakani mwa wilaya ya Arumeru na Jiji la Arusha.
Aidha majambazi hao wamekufa baada ya jambazi mmoja Sixtus Ngowi (51) ambaye alikamatwa awali kutoa ushirikiano kwa polisi kuwa anashirikiana na wenzake hao watatu raia wa Kenya.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi walipokea taarifa za Kiintelijensia Agosti 19, mwaka huu juu ya kuwepo kwa kundi la majambazi wanaotoka Kenya na wamefika mkoani humo kwa lengo la kufanya uporaji kwa kushirikiana na majambazi wenzao wa hapa nchini.
Alisema kutokana na taarifa hizo, polisi walizifuatilia na kufanikiwa kumkamata Ngowi, mkazi wa Ngulelo jijini Arusha na baada ya mahojiano ya kina alikiri kuwa yeye ni miongoni mwa majambazi hao na kwamba anashirikiana na majambazi wenzake wa Kenya na kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi hapa nchini.
Ngowi ambaye pia ni marehemu sasa, alikiri kuhusika na tukio la uporaji kwenye Kampuni ya Security Group 4 akiwa na wenzake na kuiba Dola za Marekani 2,000,000 jijini Dar es Salaam mwaka 2005 na baadaye kufikishwa mahakamani.
Lakini pia mwaka 2002, Ngowi pamoja na wenzake walihusika katika tukio la uvamizi kwenye benki ya NBC tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro na mbali na matukio hayo, Machi mwaka 2014 aliwahi kushtakiwa nchini Kenya katika Mahakama ya Sheria ya Kilimani, jijini Nairobi lakini baadaye aliachiwa huru.
Kamanda Sabas alisema kabla ya Ngowi kwenda polisi na kufanikisha mtego wa kuwakamata wenzake wa Kenya aliwataja kwa majina mmoja mmoja kuwa ni Kamau, Bon, Mike, Kim, Katiwa na wengine ambao alidai hawafahamu kwa majina lakini wanatokea nchini Kenya wakati kwa hapa nchini alimtaja mshirika wake aitwaye Richard ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam.
Mtuhumiwa huyo pia alikiri kushirikiana na wenzake kuhusika kwenye matukio ya unyang’anyi kwa kutumia silaha katika jiji la Arusha yaliyotokea Juni 23, mwaka huu na Agosti 17, mwaka huu ambapo walengwa walikuwa ni wafanyabiashara wakubwa wanaojihusisha na biashara ya madini ya Tanzanite na Hoteli za Kitalii.

Miongoni mwa wafanyabiashara hao ni pamoja na Mathias Manga ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) ambaye alijeruhiwa kwenye ubavu wa kulia kwa risasi katika jaribio la kuporwa fedha na madini na alipokuwa kwenye muendelezo wa mahojiano.
Jambazi huyo aliahidi kushirikiana na polisi kupatikana kwa wenzake.
Kamanda Sabas alisema Septemba 17, mwaka huu wakiwa kwenye mpango wa kuvamia mojawapo ya duka ya kubadilisha fedha liitwalo Sanya la jijini hapa, Ngowi alikubali kuongozana na askari kwa ajili ya kufanikisha kupatikana kwa wenzake lakini kabla ya kuwakamata walipofika eneo la Chekereni majambazi hao raia wa Kenya walishtuka kuwa walioongozana na watu waliowahisi kuwa ni polisi na ndipo walipoanza kurusha risasi ambayo ilimjeruhi mwenzao (Ngowi) aliyekuwa kwenye gari jingine iliyokuwa na polisi na kufa akikimbizwa hospitali.
Baada ya tukio hilo polisi waliamua kujibu mapigo na kufanikiwa kuwaua watu watatu ambao ni Simon Kariuki, Bonifas Mbulu na Thadeo Njuguna huku majambazi wengine wakitoroka na gari aina ya Noah lenye namba za usajili T981AVK.
Katika eneo la tukio, majambazi hao watatu kila mmoja alikutwa na bastola pamoja na risasi, mabegi matatu ya rangi nyeusi na yalipofunguliwa walikuta bunduki mbili aina ya AK 47 zenye namba 83LG 3953 56-1 na nyingine yenye maandishi ya Kirusi na SMG namba 56-128038394, bastola tatu zenye namba CZ 75 Compact Luger- 9mm, namba a.269206, CZ 85 B LUGER 9mm namba 051967 na bastola aina ya Chines namba 967741, magazini nne za ziada tupu za SMG , risasi 85 za SMG / Ak 47 na risasi 28 za bastola.
Marehemu hao watatu raia wa Kenya walikutwa na vitambulisho vitatu vya nchini Kenya vyenye majina ya Simon Kariuki, Bonifas Bulu na Thadeo Njuguna na kitambulisho kimoja cha UN-ICTR chenye jina la Chacha Marwa, leseni ya udereva iliyotolewa Kenya yenye jina la Thadeo Njuguna, kadi ya Benki ya Equity, Master kadi yenye jina la Simon Githinji pamoja na kadi ya benki ya Co-operative yenye jina la Thadeo Njuguna, simu tano aina ya Nokia, Tecno na Samsung.
CREDITY: HABARI LEO.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / POLISI YAUA MAJAMBAZI HATARI ARUSHA.

No comments :