China imeilaumu Japan kwa kukiuka
katiba na kupitisha sheria za ulinzi , ambazo zitairuhusu kupeleka jeshi
lake kupigana vita nchi za ng'ambo kwa mara ya kwaza kabisa tangu
vimalizike vita vya pili vya dunia.
Wizara ya ulinzi nchini china inasema kuwa Japan inastahili kujifunza kutokana na historia na kulinda usalama wa majirani zake.
Marekani
, uingereza na Australia , wamekaribisha mabadiliko hayo ambayo
yatairuhusu Japan kutoa mchango mkubwa katika oparesheni za kimataifa za
kulinda amani.
No comments
Post a Comment