Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MASKINI!!!!!!!!!!! KIJANA APOTEZA MAISHA KWA KUANGUKIWA NA JIWE MACHIMONI BUKOBA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Eneo la tukio husika
 
Kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Johnson Muchunguzi amefariki dunia baada ya kuangukiwa na miamba ya mawe alipokuwa katika shughuli za uchimbaji wa mchanga kwenye eneo la machimbo yasiyo rasmi ya Rwome yaliyopo katika kata ya Kashai Manispaa ya Bukoba.

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kijana huyo pamoja na wenzake walikutwa na dhahama hiyo jana majira ya asubuhi baada ya jiwe kubwa kuanguka na kumfukia wakati akiwa katika shimo alilokuwa akichimbia mchanga.

Vikosi vya usalama pamoja na kuwahi katika eneo la tukio havikuweza kuokoa maisha ya kijana huyo ,ambaye tayari alikuwa keshapoteza maisha kutokana na kuzidiwa na uzito wa jiwe moja lililomgandamiza kabla ya kufuatiwa na jiwe jingine lililokatisha tamaa juhudi za kumuokoa zilizokuwa zikifanywa na vikosi vya usalama pamoja na wananchi.

Baadhi ya Wananchi walioshuhudia pamoja na majirani wanaelezea kwa huzuni tukio hilo na kudai kuwa kijana huyo alikandamizwa na jiwe kubwa ambalo lilikuwa lizito kwan walipofika eneo la tukio walimkuta bado ni mzma akiomba msaada na kusema tukio hilo limewahuzunisha sana.

Katika hali ya kushangaza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Rwome Ponsian Wamala anakiri kuwepo kwa machimbo hayo yasiyo rasmi,huku akishindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya wachimbaji hao.

Hadi chanzo cha habari hii kinaondoka katika eneo hilo bado juhudi mbalimbali zilikuwa zikiendelea kujaribu kuutoa mwili wa marehemu Johnson kutoka katika shimo hilo.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MASKINI!!!!!!!!!!! KIJANA APOTEZA MAISHA KWA KUANGUKIWA NA JIWE MACHIMONI BUKOBA

No comments :