Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » URUSI NA MAREKANI ZAAFIKIANA JUU YA NDEGE SYRIA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Urusi na Marekani zimetia saini makubaliano yanayotarajiwa kuzuia ndege za kijeshi za nchi hizo kushambuliana nchini Syria.

Habari za kutiwa saini kwa mkataba huo zimethibitishwa na maafisa kutoka nchi zote mbili.

Urusi ilianza kushambulia kwa ndege maeneo ya Syria Septemba 30, ikisema ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS).

Wiki iliyopita, Marekani ilisema ndege za mataifa hayo zilikuwa “zimeingia eneo moja ya mapigano” na zilikuwa karibu sana kukutana.

Maafisa wa mataifa hayo wamekuwa wakitafuta mwafaka tangu mwishoni mwa mwezi Septemba.
Msemaji wa Pentagon Peter Cook amesema maelezo zaidi kuhusu makubaliano hayo yatasalia kuwa
 siri, kufuatia ombi la Urusi.

Hata hivyo, alisema mwafaka huo unaweka mikakati ya pande zote mbili kuwasiliana.
Nchi hizo mbili hata hivyo hazitaelezana habari za kijasusi kuhusu maeneo yanayolengwa na wanajeshi wa kila upande.

Bw Cook alisema mkataba huo unahakikisha ndege za kila taifa zitakaa “umbali salama” kutoka kwa ndege za taifa hilo jingine. Hata hivyo, hakueleza umbali ulioafikiwa.

Wiki iliyopita, Pentagon ilisema ndege za kijeshi za Urusi na Marekani wakati mmoja zilikuwa zimekaribiana kiasi cha marubani kuweza kuonana, kilomita 15 hadi 30.

Waziri msaidizi wa ulinzi wa Urusi Anatoly Antonov amesema makubaliano hayo yameweka mikakati ya kuzuia kushambuliana kwa ndege za Marekani na Urusi.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / URUSI NA MAREKANI ZAAFIKIANA JUU YA NDEGE SYRIA

No comments :