Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » HIVI NDIVYO KAULI YA DR.MAGUFULI INAVYOFANYIWA KAZI MKOANI DODOMA KUHUSU UHURU DAY
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na John Banda

Mkoa wa Dodoma umeanza rasmi kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli lililotaka kufanyika kwa usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya nchi siku ya tarehe 9 Disemba, 2015 kama mojawapo ya maadhimisho ya siku ya uhuru na kuwataka viongozi na wataalamu kusimamia utekelezaji wa agizo hilo. 

Uongozi wa Mkoa umeamua kuanza mapema zoezi la ufanyaji usafi pasipo kusubiri tarehe 9 Disemba na umepanga kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu likihusisha usafi wa kila siku na usafi wa siku zote za Jumamosi kuanzia saa 1:00 hadi saa 3:00 asubuhi.

Taasisi mbalimbali zilizopo Mkoani Dodoma zimetumia Jumamosi ya leo Novemba 28, 2015 kushirikiana na wananchi kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma ambapo Viongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ofisi ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wamefanya usafi eneo la Bahi Road kuelekea Nkuhungu kwa kuondoa taka na michanga kwenye mitaro ya maji ya mvua, kufyeka na kuchoma taka eneo la makaburi ya Kizota. 

Kwa mujibu wa Ratiba ya usafi iliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma-DUWASA ilifanya usafi eneo la kuanzia ofisi za waziri mkuu (Mtaa wa Mahakamani) hadi  ofisi za hazina ndogo.

TANESCO Mkoa wa Dodoma walisafisha eneo la kituo cha kuuzia mafuta cha BP Capital hadi soko la Sabasaba. 

Taasisi nyingine ni pamoja na jeshi la Magereza ambapo lilifanya usafi kuanzia mzunguko wa barabara ya kuelekea Bahi hadi maeneo ya magorofa mengi wakati mabenki yalisafisha mitaa na barabara zinazopita mbele ya majengo yao ya benki na Wakala wa Barabara TANROADS wao walisafisha kuanzia kituo cha mabasi ya mikoani hadi soko la Sarafina.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / HIVI NDIVYO KAULI YA DR.MAGUFULI INAVYOFANYIWA KAZI MKOANI DODOMA KUHUSU UHURU DAY

No comments :