Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MABWENI MAWILI YATUMIA SHILINGI MIL.8.8 SEKONDARI YA SHULE YA WASICHANA YA MSALATO DODOMA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na John Banda, Dodoma

ZAIDI ya Sh.milioni 8.8 zimetumika katika ukarabati wa sehemu ya miundombinu kwenye mabweni mawili ya Shule ya Sekondari ya wasichana Msalato mkoani Dodoma.

Fedha hizi ni michango ya Umoja wa Wanafunzi waliohitimu shule hiyo (Msalato Alumnae).

Akizungumza jana wakati wa makabidhiano ya kazi ya ukarabati huo, Mwakilishi wa umoja huo Zena Mwenge alisema ukatabati ulihusisha kuweka vigae (tiles) na kupaka rangi vyumba 14 vya vyoo vya mabweni ya Moringe na Mandela.

Aidha kufufua mfumo wa majitaka kwenye vyoo vya mabweni hayo, kuweka milango vyoo 14 na kupaka rangi ambapo kati ya vyoo hiyo 12 ni vya kuchuchumaa na viwili ni vyoo vya kukaa kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu na wasiojiweza.

Pia kuweka mfumo wa kuingiza majisafi kwenye mabweni ya Moringe na Mandera na ukarabati wa zahanati ya shule.

Alisema ukarabati pia ulihusisha kunyanyua chemba za maji machafu na kutengeneza mifereji ya kupitisha maji ya mvua yaliyokuwa yakituama nyuma ya bweni la Moringe.

Kwa upande wa zahanati wamefanikiwa kununua magodoro mapya kwa ajili na mapumziko ya wagonjwa, kutekebisha vitanda ambavyo vilishakuwa vibovu, kununua mashuka, mito  na foronya zake.

Alisema miongoni mwao wapo waliotafuta wadau kufanikisha lengo hilo na juhudi hizo zilifanikisha kupata jumla ya Sh. milioni 13.5 ambazo kati yake Milioni 5 zilitoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
na fedha hiyo ya TANAPA iliingia moja kwa moja kwenye akaunti ya shule na imehifadhiwa kwa walengo la kukarabati mabweni mengine.

Mkuu wa Shule hiyo,Mwasi Kibuni alisema majengo ya shule hiyo yako katika hali sio nzuri na kuwataka wadau mbalimbali wajitokeze kusaidia.

"Wale wenye mapenzi mema waendelee kusaidia shule hii ili kuweka shule kwenye hali inayoridhisha kwenye kujifunza na kufundishia" alisema

Alisema miaka mitatu iliyopita serikali ilitoa milioni 150 na zilitumika kwa ajili ya ukarabati wa majengo na mifumo ya majitaka pamoja na kuanza kuweka uzio kwenye shule.

Pia nyumba za walimu zilifanyiwa ukarabati pamoja na zahanati.
 
"Bado tuna safari ndefu kwani asilimia 80 ya madarasa na mabweni hayako katika hali nzuri hata kwa upande wa uzio tuna hatua ndefu ya kwenda" alisema

Baadhi ya wanafunzi Julieth Besiga wa kidato cha tano alisema wanashukuru kwa ukarabati uliofanyika kwa upande wa vyoo kwani hali ilikuwa mbaya.

Debora Robert wa kidato cha tano alisema uchafu wa vyoo ulikuwa ukiwafanya kuishi kwa hofu ya kupata magonjwa lakini baada ya ukarabati wanafunzi watafikiria zaidi kusoma na si kutibiwa.

Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony

Mavunde alisema atahakikisha anashirikiana na wadau mbalimbali ili kuondoa changamoto hizo.

Aliwataka wanafunzi waliosoma shule hiyo miaka ya nyuma warudi ili kusaidia shule yao.

Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1962.
 
mwisho

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MABWENI MAWILI YATUMIA SHILINGI MIL.8.8 SEKONDARI YA SHULE YA WASICHANA YA MSALATO DODOMA

No comments :