Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » PITIA HAPA HABARI ZA MATAIFA MBALIMBALI ZA LEO NOVEMBA 26/2015
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Unapopitia blog hii utapata taarifa mbalimbali za kitaifa kimataifa,michezo na burudani,picha na vituko vya hapa na pele lakini pia usisahau video mbalimbali pamoja na makala tofauti tofauti ....tembelea >>> KAZENZELE1.BLOGSPOT.COM

NAMIBIA 

 Namibia imeanza kuandaa mazingira ya kujiondoa kwenye Mkataba wa Roma uliobuni Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, ikidai kuwa chombo hicho ni cha kibeberu na kibaguzi. 

Haya yanajiri baada ya Baraza la Mawaziri la nchi hiyo kuidhinisha pendekezo la kujiondoa kwenye mkataba huo, lililowasilishwa na chama tawala nchini humo cha SWAPO. 

Kadhalika chama hicho cha Rais Hage Geingob kimeiagiza Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya nchi hiyo kuangalia upya sera zake za kigeni ili kutatua masuala yote ya kiufundi yatakayoweza kukwamisha mchakato huo. 

Chama hicho kimekuwa kikikariri mara kwa mara kuwa, ICC inatumika vibaya kuwadhalilisha viongozi wa bara Afrika na nchi nyinginezo zinazostawi kiuchumi.  

Hii ni katika hali ambayo, Kenya pia imekuwa ikitishia kujiondoa kwenye mkataba huo, kwa kumuandama Naibu wa Rais wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki William Ruto, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kuhusika na machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007, ambapo watu zaidi ya 1,300 waliuawa.

 Chanzo:iribuswahili
***************************************************************

 26/11/2015 >>> KENYA
 
Papa Francis ameongoza ibada ya misa ambayo imehudhuriwa na maelfu ya watu uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi ambapo amesisitiza umuhimu wa familia katika jamii.

Awali katika mkutano na viongozi wa dini mbalimbali, alisema dini haifai kutumiwa kuvuruga akisema “Mungu ni Mungu wa amani.”

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa makanisa mengine akiwemo kiongozi wa Kanisa la Kiangilikana Kenya Dkt Eliud Wabukala.

Viongozi wa dini ya Kiislamu Kenya pia wamehudhuria mkutano huo, wakiongozwa na Prof Abdulghaful El-Busaidy.

Papa Francis amesema amekuwa akihakikisha kila aendako anatangamana na watu wa dini na imani nyingine.

Wakati wa ibada ya misa ambayo ilianza saa nne asubuhi, Papa Francis alisisitiza umuhimu wa familia katika jamii na kupinga utoaji wa mimba.Watu waliohudhuria ibada hiyo walianza kuingia uwanjani mapema na walivumilia mvua ambayo ilianza kunyesha mapema asubuhi.

 Chanzo:bbcswahili

 ************************************************************

MAREKANI

Viongozi wa pande zinazopingana Sudan, hawajaunda serikali ya mpito katika kipindi cha siku 90 kama ilivyokubaliwa mwezi wa 8.

Marekani imeonya kwamba mpango huo wa amani utapata ufumbuzi pale serikali hiyo ya mpito itakapoanzishwa.

Imesema mapigano yamekuwa yakiendelea kila siku na hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya.

Maelfu ya watu wameuawa tangu Rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar walipovurugana Desemba mwaka 2013.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imezitaka pande zote kushiriki mkutano wa kwanza wa pamoja utakaofanyika siku ya Jumamosi mjini Juba.

IRAN

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran IAEO Ali Akbar Salehi amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran yaliyopewa jina la Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA yatakuwa yametekelezwa kikamilifu kufikia Januari 15 mwakani.
Ali Akbar Salehi amesema iwapo mikakati yote itaenda kama ilivyopangwa, basi makubaliano hayo yataanza kutekelezwa kuanzia mwishoni mwa mwezi ujao wa Disemba na kutamatika kufikia Januari 15. 

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran ameongeza kuwa, Tehran inaipa kipaumbele sayansi na teknolojia kwa minajili ya kuwepesisha utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi. 

Kadhalika ameashiria pia ripoti mpya ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, Yukiya Amano na kueleza kuwa ripoti hiyo ni nzuri na imeonesha kwamba Iran imetekeleza ahadi zake na hakuna ukengeukaji wowote katika shughuli zake za amani za nyuklia. 

Itakumbukwa kuwa, Julai 14 mwaka huu, Iran na nchi za kundi la 5+1 zilifikia mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama JCPOA. Kwa mujibu wa mapatano hayo yaliyotiwa saini huko Vienna mji mkuu wa Austria, Iran itapunguza baadhi ya shughuli zake za nyuklia mkabala wa kuondolewa vikwazo vya kidhalimu vya kiuchumi dhidi yake.  

Chanzo:iribswahili

 **********************************************************

26/11/2015 >>> UFARANSA

Rais Francois Hollande wa Ufaransa  leo  anatarajiwa kuwa na mazungumzo na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, ikiwa ni sehemu ya  juhudi zake  za kidiplomasia, kupata  muungano mpana zaidi katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislamu-IS, baada ya mashambulizi ya mjini Paris Novemba 13, ambapo watu 130 waliuawa. 

Kabla ya kuelekea  Moscow, Hollande  alikutana na Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi mjini Paris asubuhi ya leo. 

Rais huyo wa Ufaransa ambaye alikuweko Washington Jumanne, kwa mazungumzo na Rais Barack Obama kuhusu suala hilo, anaelekea kupata uungaji mkono mdogo hadi sasa na kampeni yake imetatanishwa na  mzozo wa kibalozi wa hivi karibuni kati ya Urusi na Uturuki. 

Uturuki iliidungua ndege ya  kivita ya Urusi inayosema ilikuwa imeingia katika anga yake na kupuuza onyo la mara kadhaa. Hata hivyo Urusi  imesema ndege hiyo ilikuwa  ndani ya Syria ikitekeleza majukumu yake ya kupambana na IS.

Hapo jana (Jumatano) katika mazungumzo na Hollande mjini Paris, Kansela wa Ujerumani  Angela Merkel, aliahidi kuiunga mkono Ufaransa katika vita vyake dhidi ya Dola la Kiislamu, na kwamba Ujerumani itatafakari jinsi inavyoweza kusaidia.

 Chanzo: dwswahili

26/11/2015 >>>> VENEZUELA

Mwanasiasa wa upinzani  nchini Venezuela amepigwa risasi  na kuuwawa  katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi, kabla ya uchaguzi wa bunge  katika muda wa karibu wiki mbili zijazo.

Luis Manuel Dias kutoka chama cha Democratic Action, alikuwa katika  mkutano  mjini Altagracia katika mkoa wa kati wa Guarico, wakati alipopigwa risasi na watu waliokuwa na silaha ndani ya gari moja .

Katibu mkuu wa chama  hicho Henry Ramos ameyashutumu makundi yenye silaha kutoka chama tawala  cha United Socialist of Venezuela kwa mauaji hayo. 

Taifa hilo la  Amerika kusini litakuwa na uchaguzi wa bunge Desemba 6.

chanzi : dwswahili 

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / PITIA HAPA HABARI ZA MATAIFA MBALIMBALI ZA LEO NOVEMBA 26/2015

No comments :