Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » HIZI HAPA HABARI ZA KIMATAIFA LEO NOVEMBA 25
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Kenya
Rais wa Kenya amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri na kuwaacha wote ambao wizara zao zilikumbwa na tuhuma za ufisadi.

Rais Uhuru Kenyatta amechukua hatua hiyo siku moja tu baada ya kutangaza ufisadi kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa. Rais ameahidi kufanya mabadiliko zaidi katika afisi yake hivi karibuni.

Katika hotuba ilioonyeshwa kwa njia ya Televisheni, Rais Kenyatta ameongeza idadi ya wizara kutoka 16 hadi 20 na kuongeza idara mpya chini ya wizara mbalimbali katika kile alichosema ni kusaidia mawaziri kutekeleza majukumu yao bora zaidi.

Idara hizo zimeongezwa kutoka 26 hadi 41.

Rais Kenyatta amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri baada ya mawaziri sita kulazimika kujiondoa kutokana na wizara walizosimamia kuhusishwa na ufisadi huku wawili kati yao wakikabiliwa na kesi mahakamani.

Ni mabadiliko yaliyotarajiwa hasa baada ya hatua ya aliyekuwa waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru kujihuzulu mwishoni mwa juma kutokana na kile alichosema ni ushauri wa daktari wake- baada ya usumbufu aliopata wizara yake ilipohusishwa na sakata kadhaa za ufisadi.

Kwa mujibu wa katiba idadi ya mawaziri inapaswa kuwa kati ya 14 na 22 na hivyo kujiuzulu kwa Bi Waiguru kulisababisha idadi hiyo kupungua hadi 13.

Baraza jipya la mawaziri linajumuisha wanawake wanne na wanaume 16.

Baadhi ya mawaziri wamesalia katika nafasi zao huku wengine wapya wakiteuliwa kuchukua nafasi za mawaziri waliohusishwa na ufisadi.

Hatua itakayofuata sasa ni kwa mawaziri wapya kuchunguzwa na kamati ya bunge kabla ya kuidhinishwa kikamilifu.

Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imekuwa ikikabiliwa na changamo ya ufisadi katika wizara kadhaa na kumekuwepo shinikizo sio tu kutoka kwa wananchi lakini pia kutoka kwa mashirika ya kijamii,viongozi wa upinzani na hata mabalozi wa nchi za kigeni kutaka hatua zichukuliwe.

Chanzo: bbcswahili

 ***************************************************************

Zimbabwe
Rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili nchini Zimbabwe. Hii ni mara ya pili kwa rais wa China kufanya ziara nchini Zimbabwe katika miaka 20 iliyopita. 

Alipohojiwa na waandishi wa habari wa China na Zimbabwe, rais Mugabe amesema,
"nataka kusema, kweli tunaisubiri kwa hamu ziara hiyo yenye maana kubwa:. 

“Rais Xi Jinping atakapokuja, tutajadiliana kuhusu miradi na mipango kadhaa, tunaitarajia China itoe misaada kwetu, ziara hiyo ya rais Xi Jinping ni mafanikio makubwa kwenye uhusiano kati ya Zimbabwe na China. Tunamkaribisha rafiki yetu mkubwa katika jumuiya ya kimataifa." 

Akizungumzia mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika nchini Afrika Kusini, rais Mugabe anaona mkutano huo utazidisha kidhahiri uhusiano kati ya Afrika na China. 

"Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika limehimiza mawasiliano kati ya China na Afrika Kusini, na mkutano huo pia utazidisha mawasiliano kati ya China na Afrika, hilo ni jambo kubwa sana. Nitashiriki kwenye mkutano huo nikiwa mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika."

Chanzo: China swahili

**********************************************************

SYRIA
Makomando maalumu wa jeshi la anga la Syria wamefanikiwa kumuokoa rubani mmoja aliyekuwa anashikiliwa na wanachama wa kigaidi nchini humo. 

Jeshi la Syria limetangaza kuwa, baada ya jeshi la Uturuki kushambulia na kuidungua ndege ya kijeshi ya Russia na kutekwa nyara mmoja wa marubani wake wawili na wanachama wa kigaidi hapo jana, timu maalumu ya makomando wa jeshi la anga la Syria walianzisha operesheni kali ya kumuokoa rubani huyo operesheni ambayo imeweza kuzaa matunda. 

Tayari rubani huyo amepelekwa kambi ya kijeshi iliyo karibu na mji wa Lattakia nchini Syria. 

Hii ni katika hali ambayo hapo jana saa moja baada ya kutangazwa kudondoshwa ndege hiyo ya Russia, makundi ya wabeba silaha sanjari na kuonyesha picha za rubani huyo, yalidai kuwa yamemuua. 

Jana jeshi la anga la Uturuki kwa kutumia kombora la anga kwa anga, lilishambulia ndege hiyo ya kivita ya Russia aina ya Sukhoi Su-24 iliyokuwa ikipaa katika mpaka wa Syria kwa madai kuwa, eti ilikuwa imevuka mpaka wa Syria na kuingia Uturuki. 

Wizara ya Ulinzi ya Russia umetangaza kuwa ndege hiyo ilikuwa ikiruka katika anga ya Syria na kamwe haikuingia anga ya Uturuki. 

Kufuatia hujuma hiyo, Russia imekitaja kitendo hicho kuwa cha uchokozi na tayari imetangaza kukata uhusiano wa kijeshi na Uturuki.

Chanzo: Iribswahili

Tunisia

Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia ametangaza hali ya hatari ya siku 30 kufuatia shambulizi dhidi ya basi lililokuwa limewabeba maafisa usalama wa nchi hiyo hapo jana. 

Rais Essebsi amechukua hatua hiyo kupitia hotuba aliyoitoa kufuatia shambulio hilo, ambapo sambamba na kulaani hujuma hiyo ya kigaidi, ametangaza hali ya kutotoka nje kuanzia saa tatu za usiku hadi saa 11 alfajiri.

Akisisitiza kuwa, hivi sasa Tunisia iko katika vita dhidi ya ugaidi, amesema kuwa kufuatia hali hiyo serikali imejizatiti kulipatia jeshi la nchi hiyo kila aina ya zana zitakazotumika katika vita hivyo. 

Kwa mujibu wa duru za ikulu ya rais wa Tunisia, askari 20 wa gadi ya rais wameuawa katika shambulizi hilo la kujiripua lililolenga basi la askari hao. 

Inaelezwa kuwa, mtu aliyekuwa amevalia mada za miripuko alikuwa ndani ya basi hilo kabla ya kujirupua na kusababisha maafa hayo hapo jana. 

Tunisia imekuwa ikikumbwa na vitendo vya kigaidi huku raia wake wengi wakiwa ndio wanaounda asilimia kubwa ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh huko nchini Iraq na Syria.

Chanzo: Iribswahili

********************************************************

Uturuki 

Jumuia ya kujihami ya nchi za magharibi NATO imesema inasimama pamoja na Uturuki baada ya kuitungua ndege ya kivita ya Urusi.

Akizungumza baada ya mkutano wa dharura ulioitishwa na Uturuki, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema tathmini ya tukio hilo inaonyesha kuwa ndege ya kivita ya Urusi iliruka katika anga ya Uturuki.

Huku kukiwa na hali ya wasiwasi, Stoltenberge ametaka kuwepo na hali ya utulivu kutoka pande zote.
Amesema taarifa walizozipokea kutoka nchi washirika, zinaenda sambamba na maelezo ya Uturuki ya tukio hilo.

"Ushirikiano tulioupata kutoka kwa washirika mbalimbali kwa leo unathibitisha taarifa tuliyoipata kutoka Uturuki."

Hata hivyo, Moscow bado wanasisitiza kwamba, ndege hiyo ilikuwa katika anga ya Syria, na kwamba hakukuwa na ukiukwaji wa anga ya Uturuki.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema kila mtu sharti aheshimu haki ya nchi yake ya kulinda mipaka yake.

Rais Obama pia ameitetea haki ya Uturuki ya kulinda anga yake.

Kwa upande wake, msemaji wa jeshi la Urusi, Jenerali Sergey Rudskoi, amesema angalau rubani mmoja kati ya wawili wa ndege hiyo iliyoangushwa na Uturuki siku ya Jumanne amefariki kutokana na moto uliokuwepo chini baada ya kutoka katika ndege hiyo.

Mpaka sasa hakijulikani kilichomsibu rubani mwengine.

Chanzo :Bbcswahili

*****************************************************

Ubelgiji 

Usafiri wa treni kwa njia za chini ya ardhi katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels ulitarajiwa kufunguliwa tena leo, baada ya kufungwa kwa siku kadhaa katika operesheni zenye uhusiano na mashambulizi ya kigaidi mjini Paris. 

Hali kadhalika shule na chekechea zilizokuwa zimesimamishwa, zitaendelea na shughuli kama kawaida. 

Wakati huo huo uchunguzi umeendelea kumtafuta mtu anayeshukiwa kuhusika katika mashambulizi ya mjini Paris tarehe 13 mwezi huu wa Novemba, baada ya kuibuka video iliyonaswa na kamera kwenye kituo cha kujaza mafuta karibu ya Paris unaomuonyesha mtu huyo  akiwa katika gari lililotumiwa katika mashambulizi hayo. 

Mshukiwa huyo anafikiriwa kuwa mtu hatari, ambaye huenda amejihami kwa silaha.

Chanzo: Dw Swahili

Urusi.

Urusi imeonya kuwa italipiza kisasi kufuatia kuangushwa kwa ndege yake.

Waziri mkuu wa Urusi , Dmitriy Medvedev, amesema kuwa Uturuki inawalinda Islamic State .

Medvedev amedai kuwa Uturuki inahofia kupoteza kipato kikubwa inachofaidika kutokana na wizi wa mafuta kutoka Syria.

Aidha, Medvedev amedai kuwa mikataba yote na Uturuki imesimamishwa na kuwa kampuni zote zenye asili ya Uturuki zimepigwa marufuku nchini Urusi.

Hayo yamejiri huku rais wa Marekani Barack Obama amemhakakishia mwenzake rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa nchi yake inaiunga mkono Uturuki katika jitihada za kulinda mipaka yake.

Hakikisho hilo la rais Obama linafwatia hatua ya Uturuki kuidungua ndege ya Urusi karibu na mpaka wa Syria.

Mataifa yote duniani yalihofia kutibuka kwa vita iwapo Moscow ingelipiza kisasi kufuatia mauaji ya askari wake katika shambulizi hilo.

Ikulu ya WhiteHouse ilisema kuwa wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu kati ya marais hao wawili kuwa wote walikubaliana kutuliza hali hiyo.

Umoja wa mataifa na muungano wa kujihami ya nchi za Maghraibu NATO wamewataka Urusi na Uturuki kutuliza hasira zao.

Akizungumza baada ya mkutano wa dharura wa mataifa ya NATO ulioitishwa na Uturuki, katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema tathmini ya tukio hilo inaonyesha kuwa ndege ya kivita ya Urusi iliruka katika anga ya Uturuki.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / HIZI HAPA HABARI ZA KIMATAIFA LEO NOVEMBA 25

No comments :