Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » WAKAZI WA BAHI WAAMUA KUOMBA JUU YA UPATIKANAJI WA DARAJA KUOKOA SHUGHULI ZA KIJAMII IKIWEMO ELMU WILAYANO HUMO
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na Peter Mkwavila,denis kazenzele 

WANANCHI wa vijiji vya Chikola Maghomanje na Nhgulugano wilayani Bahi mkoa wa Dodoma wanatarajia kufanya ibada ya pamoja kumwomba Mungu ili watu waweze kuguswa kusaidia ujenzi wa daraja lililokatika kwa mwaka mmoja.

Aidha pamoja na maombi hayo pia wananchi hao watamshukuru mungu kwa kuwezesha uchaguzi kufanyika kwa amani ikiwemo na ipatikanaji wa viongozi kwa njia ya amani pia.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao wa vijiji hivyo Mchungaji wa kanisa la Angalikan Chikola Peter Fumbi alisema maombi hayo yatafanyika kwa ajili ya kumomba mungu ili zipatikane fedha zitazowezesha ujenzi wa daraja hilo.

Fumbi alisema kuwa jumla ya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 300 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo,hivyo kwa kupitia maombi hayo wanaamini fedha hizo zitapatikana.

Alisema kwa hivi sasa baada ya kukatika kwa daraja hilo kumekuwepo na shida kubwa ikiwemo na kukosa huduma ya kuwasafirisha wagonjwa wakiwemo wajawazito wanaotakiwa kupelekwa Hospitali ya mkoa.

Aidha kero nyingine ya kukosekana kwa daraja hilo ni pamoja na wanafunzi wanaotoka kijiji cha Chimendeli  kuja shule ya chikola sekondari kushindwa kuvuka  pindi wanapokuta maji yamejaa.

Hata hivyo mchungaji huyo alisema kuwa mvua za masika zinakuja kuna hatari ya wananchi wakakosa huduma za kimsingi kwa kuwa hawatakuwa na mawasiliano yoyote ya barabara kutokana na kukatika kwa daraja hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Chikola Petro Masaka akizungumza na waandishi wa habarialisema kuwa maombi hayo yatawashirikisha watu wote bila kujali itikadi zozote za kidini na vyama vya siasa.

Masaka alisema kuwa ili kukamilika daraja hilo tunahitaji nguvu za ziada kutoka kwa wahisani,watu binfsi hata na kwa serikali pia.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / WAKAZI WA BAHI WAAMUA KUOMBA JUU YA UPATIKANAJI WA DARAJA KUOKOA SHUGHULI ZA KIJAMII IKIWEMO ELMU WILAYANO HUMO

No comments :