Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » SHAHIDI WA PEMBE ZA FARU ZA WACHINA MBEYA ASEMA YAKE MAHAKAMANI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

picha ikionesha pembe za ndovu{ sio halisi za tukio husika}

habari kutoka mbeya

SHAHIDI wa Kwanza katika kesi inayowakabili raia wanne wa Kichina wanaokabiliwa na kesi ya kukamatwa na nyara za Serikali ikiwa ni Pembe za Faru ameieleza Mahakama jinsi watuhumiwa hao walivyokutwa na nyara hizo.

Shahidi huyo Godliving Mollel(36) Afisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Kasumulu wilayani Kyela akiongozwa na Wakili wa Serikali Archiles Mulisa akisaidiana na Wankyo Saimon mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mbeya, Michael Mteite alisema watuhumiwa hao walikamatwa Novemba 11, mwaka huu majira ya saa mbili na nusu asubuhi Kasumulu wilayani kyela.

Shahidi huyo alieleza mahakama kuwa siku hiyo ya Novemba 11 Raia hao walielekea moja kwa moja katika dirisha la uhamiaji na baadaye mmoja wao aliyemtambua kwa jina la Song Le alienda kwenye dawati la Forodha akiomba kupatiwa Hati halisi ya gari kwa kuwa ilibaki wakati ikipita awali ndipo alipogundua kuwa ni gari iliyoruhusiwa Septemba 26.

Alisema baada ya Raia huyo ambaye alimtambua kama ndiye mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo alimuomba nyaraka ili ajiridhishe kama ameingia kihalali nchini na ndipo alipokagua na kujiridhisha na kumgundua kuwa ndiye aliyekuwa mmiliki wa Gari lililopitishwa na Zhang Peng.

Alisema wakati akitaka Hati yake ya gari Mshtakiwa huyo alikuwa na haraka pamoja na wasiwasi jambo ambalo lilimfanya amtilie shaka na kukumbuka mazingira yaliyopitishiwa gari siku ya mwanzo.

Mollel alizidi kuiambia Mahakama kuwa alipokuwa akielekea kwenye Chumba cha kuhifadhia Nyaraka Mshtakiwa alizidi kumfuata na kumsisitiza kuhusu muda jambo ambalo lilipelekea kupiga Simu kwa Askari Polisi akimuomba aje ili walifanyie ukaguzi Gari hilo kabla ya kumkabidhi.

Alisema baada ya kupata Nyaraka alizokuwa akizihitaji Song le alimsubiri Askari ambaye alipofika walimwamuru Mshtakiwa kupeleka gari sehemu maalum ya ukaguzi huku akiwa sambamba na Maafisa wa Uhamiaji, Polisi na Afisa Forodha lakini kabla ya kuanza upekuzi Afisa Uhamiaji aligundua kuwa wengine hawapo aliofika nao kusaini Pass za kuingilia nchini.

Alisema baada ya kuwafuata watu hao ambao ni washtakiwa Xiao Shaodan, Chen Jianlin na Hu Liang ambapo hakuwakuta na kuamuru kupiga simu Kyela na Tukuyu ili waweze kuzuiliwa endapo watakuwa wametoroka.

Alisema baada ya dakika 40 washtakiwa walikamatwa wakiwa kwenye gari aina ya Kosta likitokea Kyela kuelekea Mbeya na baada ya kufikishwa kwenye eneo la ukaguzi upekuzi ulianza kwa kila mmoja kutoa begi lake na kulishika na ndipo fundi alipoitwa kwa ajili ya kulifungua gari katika baadhi ya maeneo kwa maelekezo ya askari polisi.

Alisema katika upekuzi huo waligundua katika buti ya gari mahali ambapo pamechomelewa na kasha kufungiwa nati kwa chini kama tenki la mafuta na baada ya kulifungua ndipo walipokuta vitu vimefungwa vinavyodhaniwa kuwa ni pembe za Faru zikiwa 11.

Aliongeza kuwa ndipo aliposaini hati ya upekuzi ya Polisi kama shahidi wa kwanza na ndipo Maafisa Wanyapori walipoitwa na kugundua kuwa ni Pembe za Faru zilizokuwa zikitoka Nchini Malawi na kuingia nchini Tanzania.

Hata hivyo Wakili wa Serikali alipomaliza kumuongoza shahidi wa Kwanza, Wakili wa Utetezi alimuomba Hakimu Mkazi Michael Mteite kuahirisha kuendelea kutolewa ushahidi kwa kuwa muda ulikuwa umeisha na Washtakiwa walipaswa kuwa Gerezani kwa ajili ya Chakula na Mapumziko.

Hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa Serikali Wankyo Saimon ambaye alidai kuwa kwa mujibu wa makubaliano walipaswa kupokea ushahidi kutoka kwa mashahidi watano na kesi hiyo ilipaswa kuisha kwa muda wa siku mbili kutokana na kuwa na mlengo wa kitaifa hivyo akamuomba Hakimu kuendelea na ushahidi.

Kutokana na Maelezo hayo Hakimu Mkazi Mteite alikubalina na hoja ya upande wa Utetezi kuwa muda umeisha kutokana na upande wa mashtaka kutumia muda mrefu wa siku nzima kueleza upande wao hivyo kuwanyima washtakiwa kuuliza maswali pamoja na wakili wao hivyo kuamuru kuahirisha kesi hiyo hadi siku inayofuata.

Awali Molel alisema Septemba 26, mwaka huu  mtu mmoja raia wa China aliyefahamika kwa jina la Zhang Peng akiwa na gari aina ya Toyota Hilux yenye namba za usajili T 103 DER alifika kuomba kibali kwa ajili ya kwenda nchini Malawi ambapo alipitia taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuonesha vielelezo vyote vinavyotakiwa.

Alisema katika nyaraka alizokuwa nazo dereva huyoi akabainika kuwa hakuwa mmiliki wa gari wala kuwa na kibali kutoka kwa mwenye gari jambo ambalo alifuatilia kwa kutumiwa barua kutoka kwa mmiliki kwa njia ya mtandao kupiti email yake barua iliyotoka kwa mshtakiwa namba moja Song Lei.

Alisema baada ya kumaliza kupitia nyaraka zote alimwamuru dereva huyo kupeleka gari eneo maalumu la ukaguzi ambapo katika upekuzi huo akiwa ameambatana na maafisa wengine walipata wasiwasi kwenye buti ya hiyo gari baada ya kugundua kuwepo kwa eneo lililofungwa kwa kutumia nati na kuchomelewa.

Alisema baadaye aliamriwa kufunguliwa kwa eneo hilo ambapo dereva alikuwa na mtu mmoja ambaye ni raia wa Malawi alifika na Bisibisi kwa ajili ya kufungua na baada ya kufunguliwa waligundua kuwepo kwa tenki linguine ndani kiwa limechomelewa kama tenki la kuhifadhia mafuta lakini baada ya kulipekua pia halikuwa na kitu chochote ndani.

Shahidi huyo aliongeza kuwa baada ya kujiridhisha na upekuzi huo Dereva huyo aliandikiwa kibali cha muda cha siku tisini kwa ajili ya kwenda Malawi na kwamba kabla ya hapo walikubaliana kufanya upekuzi wa kina pindi dereva huyo atakapokuwa akirejea nchini.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / SHAHIDI WA PEMBE ZA FARU ZA WACHINA MBEYA ASEMA YAKE MAHAKAMANI

No comments :