Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » KISPORTS ZAIDI ASUBUHI YA LEO, USAJILI WA YANGA DIRISHA DOGO, ORODHA YA 11 BORA UEFA BARCA WAMO HATA MMOJA?MAREFA WATAKAOCHEZESHA EURO WAMETAJWA NA JE MOURINHO ANASEMAJE BAADA Y AVIPIGO????...FUNGUA HAPA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

SPORTS
Rasmi Yanga imekibomoa kikosi cha Mwadui FC baada ya kumnasa mshambuliaji wake, Paul Nonga.

Nonga amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, leo.

Awali Nonga alisafirishwa na Yanga kutoa Mwadui, Shinyanga kwa ajili ya kumalizia mazungumzo na mambo yamekamilika leo.

Kabla ya kujiunga na Mwadui FC, Nonga alikuwa mmoja wa washambuliaji hatari wa Mbeya City chini ya Juma Mwambusi ambaye sasa ni kocha msaidizi wa Yanga na inaelezwa ndiye aliyempendekeza.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Kocha wa Simba, Dylan Kerr amesema ataendelea kumtumia mshambuliaji wake Danny Lyanga kama mshambuliaji wa kati ili kumpa nguvu zaidi ya kufanya vizuri.

Kerr amesema, Lyanga anapaswa kucheza mechi zaidi ili aongeze hali ya kujiamini na kufanya vizuri zaidi.

Lyanga amekuwa gumzo baada ya kuichezea Simba mechi moja tu dhidi ya Azam FC ambayo aliipeleka mchamchaka.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Kikosi bora cha wachezaji kumi na moja kilichocheza hatua ya makundi ya michuno ya klabu bingwa ulaya kimetangazwa na Uefa.

Washambulia Cristiano Ronaldo, wa Real Madrid,Hulk anayekipiga na klabu ya Zenit St Petersburg's pamoja na Thomas Muller wa Bayern Munich ndio wanaongoza safu ya ushambuliaji kikosi hicho kikitumia mfumo wa 4-3-3.

Ligi Kuu England imetoa wachezaji wawili, sawa na ligi ya Ujerumani na ile ya Ufaransa.
Mabingwa Watetezi wa kombe la klabu bingwa ulaya Barcelona, hawatoa hata mchezaji moja katika kikosi hicho licha ya kuwa na safu kiwembe ya ushambuliaji.

Kikosi kamili ni:

Kipa ni Kevin Trapp (Paris Saint-Germain
Mabeki ni kulia: Andrea Barzagli (Juventus)Thiago Silva (Paris Saint-Germain)Diego Godin (Atletico Madrid) David Alaba (Bayern Munich)
Viungo ni Sven Kums (Gent) Willian (Chelsea) Raheem Sterling (Manchester City)
Washambuliaji ni Thomas Muller (Bayern Munich) Hulk (Zenit St Petersburg) Cristiano Ronaldo (Real Madrid

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Kamati ya Marefa ya shirikisho la soka barani ulaya Uefa imeteua waamuzi 18 kwa ajili ya michuano ya ulaya itakayofanyika huko nchi Ufaransa mwaka 2016.
Waamuzi hao watachezesha michezo 51 ya michuano hiyo ya ulaya itakayoanza kutimua vumbi kuanzia June 10 na kumalizika Julai 10 mwaka 2016.
Katika kila mchezo mmoja watatumika waamuzi watano kama iliyokua katika michuano ya Euro ya mwaka 2012, kutakua na mwamuzi wa kati akisaidiwa na waamuzi wawili wa pembeni na wengine wawili katika kila goli.
Orodha ya mwisho ya waamuzi watakaochezesha fainali hizo itatolewa mwezi Februari mwakani na kamati hiyo ya waamuzi.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Siku chache baada ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya Leicester City , mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho sasa anadai wachezaji wanamsaliti

Mourinho anasema wamefanya kila jitihada katika mazoezi kuhakikisha kuwa the blues wanaibuka videdea lakini wapi !

''Inachosha sana kutizama kazi ambayo tumefanya ikisalitiwa'' alisema Mourinho.

''Moja ya vipawa vyangu tajika ni uwezo wa kusoma na kuelewa mchezo kwa haraka,,hii ndio nahisi nimesalitiwa''

''Wakati mwengine nahisi kama vile nilijitahidi kuimarisha uwezo wa wachezaji wetu msimu uliopita na sasa inaonekana wameshindwa kustahimili ushindani katika kiwango hicho''alifoka Mourinho.

Msimu uliopita Chelsea walipoteza katika mechi tatu tu walizoshiriki lakini msimu huu, mambo yamewageuka na maji yamezidi unga.

Chelsea walipoteza mechi yao ya 9 msimu huu kati ya 16 walizocheza.

The Blues sasa wamejipata katika nafasi ya 16 wakiwa na alama moja tu zaidi ya timu zinazotishiwa kushushwa daraja msimu ujao.

Hata hivyo kinachomkera sana raia huyo wa Ureno ni kichapo cha 2-1 mikononi mwa vinara wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City.

Mabao ya Jamie Vardy na Riyad Mahrez yaliisaidia 'The Foxes' katika uwanja wao wa nyumbani wa King Power Stadium.

Kinachowashangaza wapenzi wa timu hiyo ni kwanini wachezaji walioishinda ligi msimu uliopita sasa wanashindwa hata kustahimili ushindani kutoka kwa timu ndogo.

Iwapo motisha katika timu ya Chelsea haitaimarika kwa haraka kuna hofu kibarua cha mreno huyo kitaingia mchanga.

Kocha huyo wa Chelsea anakila sababu ya kuwa na hofu haswa wakijiandaa
kukabiliana na Sunderland siku ya jumamosi.

Mourinho amekiri kuwa sasa haitawezekana kwa the Blues kufuzu kwa kinyang'anyiro cha kuwania kombe la mabingwa barani ulaya mwakani.

''Hatuwezi maliza katika nafasi 4 za kwanza ila tukijitahidi huenda tukacheza katika ligi ya Europa'' alisema Mourinho.

'Naona haya bila shaka'

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / KISPORTS ZAIDI ASUBUHI YA LEO, USAJILI WA YANGA DIRISHA DOGO, ORODHA YA 11 BORA UEFA BARCA WAMO HATA MMOJA?MAREFA WATAKAOCHEZESHA EURO WAMETAJWA NA JE MOURINHO ANASEMAJE BAADA Y AVIPIGO????...FUNGUA HAPA

No comments :