Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » ZA KIMATAIFA ASUBUHI YA LEO DISEMBA 16/2015 HIZI HAPA....
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

MEXICO
Miili ya watu wapatao 19 imepatikana katika jimbo la Mexico la Guerrero, ambako wanafunzi 43 walitoweka mwaka jana.
Polisi wanasema miili hiyo ilitupwa kwenye mto mwembamba, wenye kina cha mita mia tano katikati ya miamba na miti karibu na kijiji cha Chichi-hua-lco.
Miili nane kati ya hiyo ilikuwa inaonekana kuchomwa baadhi ya viungo.
Vipimo vya DNA vinatarajiwa kuchukuliwa kutoka katika familia za wanafunzi hao waliokufa, kuweza kujua kama ni kweli ni hao, ambao hawajapatikana mpaka sasa.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

COLOMBIA
Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos amesema makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na waasi wa FARC ni hatua kubwa katika juhudi za kufanikisha kutiwa saini kwa mkataba wa amani mwezi Machi mwakani.
Akihutubia kwa njia ya televisheni, Rais Santos amesema pande hizo mbili zimeafikiana katika mambo manne kati ya matano.
Makubaliano haya ya sasa yanawaweka waathirika wa mzozo wa nchini humo katika hali ya matumaini ya kufikiwa kwa mchakato wa amani.
Watu takriban 200,000 wamepoteza maisha kutokana na mzozo na wengine milioni sita wanakadiriwa kuyakimbia makazi yao.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

ZIMBABWE
Mbunge mmoja wa chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe amefikishwa kortini kujibu tuhuma za kumvunjia heshima mke wa Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo.

Mbunge Justice Wadyajena anadaiwa kumtusi Bi. Grace Mugabe wakati wa mkutano wa chama hicho katika mji wa Victoria Falls. "Ondoka hapa wewe mjinga kama huyo 'Mama' yako", Wadyajena anasemekana alimwambia mwanachama mwingine wa ZANU-PF aliyekuwa amevalia fulana yenye picha ya Bi. Grace.

Mke wa Rais wa Zimbabwe amepewa jina la 'Mama' ndani ya chama tawala na inasemekana kuwa ana ushawishi mkubwa mno ndani ya chama hicho na kwenye serikali kwa ujumla.

Ingawa wengi wameiona kesi hiyo kama ya kipuuzi, wachambuzi wa masuala ya sheria wanasema mbunge Justice Wadyajena anaweza kupoteza nafasi yake ya ubunge endapo atapatikana na hatia.

Rais Robert Mugabe ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 amekuwa akiwachukulia hatua kali wanasiasa wanoonekana kuingilia masuala ya familia yake. 

Wadadisi wanasema mkwaruzano kati ya Grace Mugabe na makamu wa zamani wa Rais, Joyce Mujuru ndiyo iliyomfanya Rais Mugabe kumpiga kalamu Bi. Mujuru mwaka uliopita.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

GENEVA

Pande zinazo zozana Yemen zimeanza mazungumzo ya kutafuta amani leo mjini Geneva, Uswisi katika juhudi za kuutafutia ufumbuzi mzozo wa Yemen huku makubaliano ya kusitisha mapigano yakianza kutekelezwa.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Ahmad Fawzi amewaambia wanahabari kuwa mazungumzo hayo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa yanalenga kupatikana kwa suluhisho la kudumu kuhusu mzozo wa Yemen kwa kutoa mazingira salama ya kibindamu, kusitisha mapigano na kurejea kwa utawala wa amani na unaoeleweka kisiasa.

Juhudi za hapo awali za kuutatua mzozo huo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 5,000 zilishindwa kuondoa tofauti za pande zinazozana. Fawzi amesema washauri sita na wajumbe 12 wanashiriki katika mazungumzo hayo.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

KENYA

Kenya ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa shirika la kimataifa la biashara WTO imesema mawaziri wa biashara wanaokutana katika mkutano huo wa siku nne ulioanza leo mjini Nairobi, wanapaswa kuamua iwapo shirika la WTO liendelee kusimamia makubaliano makubwa ya kibiashara ambayo yanaonekana kuwa magumu kufikiwa.

Shirika hilo lenye makao yake mjini Geneva na ambalo lina zaidi ya nchi wanachama 160 limekuwa likijaribu kufikia makubaliano ya kibiashara mapana na makhususi ya kuondoa vizuizi vya kibiashara tangu mkutano wa Doha mwaka 2001 bila ya mafanikio makubwa.

Lengo la mkutano huo wa Nairobi ni kuamua ni jinsi gani WTO itasonga mbele baada ya miaka kadhaa ya kutoweza kupiga hatua ya maana.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed amesema shirika hilo halijawa la tija kwa wanachamna wake hasa nchi zinazostawi ambazo zitanufaika iwapo vikwazo vya kibiashara vitaondolewa ili kuweza kufikia soko la kimataifa bila ya masharti magumu mno.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

UJERUMAN

Polisi wa Ujerumani wamemkamata mmoja wa wahubiri mashuhuri wa kiislamu kwa madai ya kuliunga mkono kundi la kigadi linalopigana nchini Syria.

Mhubiri huyo raia wa Ujerumani kwa jina Sven Lau mwenye umri wa miaka 35 anashutumiwa kwa kuunga mkono vitendo vya kigaidi na kuwasajili wapiganaji kwa ajili ya kundi lenye makao yake Syria la Jaish al Muhajireen wal Ansar ambalo Ujerumani imeliorodhesha kama kundi la kigaidi.

Waendesha mashitaka wamesema mwaka 2013, Lau alikuwa mwakilishi wa kundi hilo nchini Ujerumani na aliwasajili watu wawili kujiunga na kundi hilo na pia anashitakiwa kwa kutuma euro 250 kwa mpiganaji raia wa Ujerumani aliye Syria.

Lau amekamatwa katika jimbo la North Rhine Westphalia.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

UTURUKI

Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema uhusiano kati ya nchi yake na Umoja wa Ulaya umeimarika pakubwa tangu mkutano wa kilele kati ya Uturuki na Umoja huo uliofanyika hivi karibuni.

Katika mkutano wa pamoja na Waziri mkuu wa Bulgaria mjini Sofia, Davutoglu amewaambia wanahabari kuwa ukurasa mpya umefunguliwa kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya baada ya kipindi cha miaka minne.

Umoja wa Ulaya hapo jana ulianza kushughulikia mchakato wa nchi hiyo kujiunga na Umoja huo kama mwanachama ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kusaidia kuukabili mzozo wa wahamiaji barani Ulaya.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

UCHINA
Barua iliyoandikwa na kiongozi wa chama cha Kikomunisti cha Uchina Mao Zedong akimwandikia kiongozi wa chama cha Leba cha Uingereza imeuzwa £605,000 ($918,000) kwenye mnada.
Kwenye barua hiyo ya mwaka 1937, Mao anamuomba Clement Attlee usaidizi katika kukabiliana na wanajeshi wa Japan waliokuwa wamevamia Uchina.
Wanadi wa bidhaa Sotheby wamesema barua hiyo ni ya thamani kubwa kutokana na saini ya Mao.
Bei ya mwisho ilizidi sana bei iliyotarajiwa ya £100,000-150,000.
Mnunuzi ni raia wa Uchina anayekusanya vitu vya kale.
Mao Zedong alizaliwa 1893 na ni mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Kikomunisti cha Uchina na mwanafalsafa msifika wa karne ya 20.Alisaidia kuunga jeshi la Uchina kwa jina Red Army, na kuwaongoza kutembelea maili 6,000 kutoroka maadui wao.
Baada ya ushindi 1949, Mao alitangaza kuundwa kwa Jamhuri ya Watu wa Uchina na akawa kiongozi wa kwanza. Sera zake zilisababisha vifo vya mamilioni ya watu.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / ZA KIMATAIFA ASUBUHI YA LEO DISEMBA 16/2015 HIZI HAPA....

No comments :