Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » CCWT CHEMBA CHALALAMIKIA HALMASHAURI KUWATOZA MICHANGO ISIYOSTAHILI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na John Banda, Chemba
 
CHAMA cha wafugaji (CCWT) wilayani Chemba mkoani Dodoma kimelalamikia kitendo cha watumishi wa halmashauri hiyo kuwatoza fedha za michango mbalimbali ikiwemo  mfuko wa maendeleo ya elimu kwa kutumia stakabadhi feki zinazo changia kupotea kwa mapato ya serikali.

Wafugaji hao waliyasema hayo juzi wakati wakizungumza na na Jambo leo wilayani hapa.
Katibu wa chama hicho wilayani hapa Saidi Nghambi, alisema kuwa watendaji wa vijiji mbalimbali wamekuwa wakiwatoza pesa za mchango huo wa mfuko wa jimbo kwa kutumia stakabadhi feki tofauti na zile za halmashauri hali inayosababisha upotevu wa mapato ya ndani.

Nghambi alisema kuwa watendaji wa vijiji wilayani hapa pamoja na wale wa vitongoji na vijiji wamekuwa wakichangisha michango hiyo kwa kutumia stakabadhi za madukani ambazo hazina muhuri wala nembo ya halmashauri.

“Tunachangishwa lakini stakabadhi unayopewa ni ile ya dukani kama zile tunazo pewa na wauzaji wa maduka ya vifaa vya ujenzi au vyakula”alisema Nghambi.

Aidha alisema kuwa wamekuwa wakilalamika katika ngazi mbalimbali pamoja na kupeleka ushahidi wa stakabidhi hizo ambazo zinatumiwa na watendaji hao lakini hakuna hatua zilizo chuliwa hadi hivi sasa.

“Tuliandika barua kwenda kwa waziri mkuu wakati ule wa serikali ya awamu ya nne, mkuu wa mkoa wa Dodoma akapewa jukumu la kulishughulikia suala hili lakini hadi hivi sasa hakuna hatua zilizo chukuliwa”alisema Nghambi.

Alisema kuwa pamoja na kuchangishwa michango hiyo lakini hakuna sheria iliyopitishwa na vikao vya halmashauri kuwataka kuchangia mchango huo wa mfuko wa elimu.

“Hiki kinachofanyika ni kile kinachotokana na sheria za wilaya tuliyotengana nayo ya Kondoa lakini sisi hapa bado hatuna sheria hiyo ya mfuko wa elimu” alisema Nghambi.

Naye mwenyekiti wa chama hicho cha wafugaji Salamba Mataji, alisema kuwa hali hiyo imekuwa kero kwao kutokana na kuchangishwa michango mingi lakini stakabadhi wanazopatiwa ni feki.

“Tulishakwenda hadi kwa mkurugenzi lakini hakutusikiliza na kutuambia sisi wafugaji wajinga na kutufukuza bila kutusikiliza”alisema Mataji.

Mataji alisema kuwa hivi sasa wanajipanga kumwandikia barua Rais Dk, John Magufuli ili aweze kuwasaidia katika kuondokana na adha hiyo ambayo wameipata kwa kipindi kirefu.
“Wafugaji wa Wilaya hii tumenyanyasika kwa muda mrefu sana hivyo basi tunataka kwenda kumuona mweshimiwa Rais”alisema Mataji.

Akijibu malalamikoa hayo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dk, William Mafwele, alisema kuwa suala la kuwepo kwa sheria ya mfuko huo wa elimu tayari lilishapitishwa na baraza la madiwani.

“Kama ni suala la sheria ipo ila hilo suala la stakabadhi feki ambazo watendaji wanazitumia kwa kuwapatia wafugaji hilo ni kosa la jinai na wafugaji wanatakiwa wakatae kutoa fedha zao kama hakuna stakabadhi zinazotambulika na halmashauri ”alifafanua Dk Mafwele
 
Mwandishi:John Banda
 
Mhariri: Denice J. Kazenzele
 
January /27/2016

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / CCWT CHEMBA CHALALAMIKIA HALMASHAURI KUWATOZA MICHANGO ISIYOSTAHILI

No comments :